Mkiambiwa mashabiki wa Asenyo bado mko na utoto mwingi mnakasirika.
Sasa hapo mwenyewe unafurahia kabisa kuona timu yako inaingia kwenye goli la mpinzani wako zaidi ya mara 75 na n kuishia kupata vigoli vitatu, halafu mpinzani wako anaingia mara 13 tu golini kwako na kukushona goli 2 huoni kama foward yako ni mbovu kiwango cha kutupwa?
Kumbuka pia jinsi hayo magoli yalivyofungwa.
La kwanza, mpemba Rashidi alipiga move kali na shuti amazing la nje ya box akapata goli.... against the run of play. Na kama sikosei, Chidi ndiye alikuwa mchezaji aliye mbele zaidi Kwa Manyumbu, huku wengine wamepaki basi Kwa hofu kubwa wakijiandaa kujilinda na shambulio tulilokuwa tunawapelekea, hivyo hakuwa na msaada. Tukapoteza mpira, mpemba akafanya yake. Lilikuwa goli Bora sana Kwa kweli.
La pili ndilo lilifungiwa ndani ya box. Na lenyewe pia lilikuwa la kimiujiza miujiza hivi. Yaani Kona imepigwa, ikawa cleared kidogo tu ndani ya box, tukaanza kujipanga kupiga counter moja hatari sana, mara akatokea Martinez na diving header ya mpira ulio kima Cha mbuzi, mpira ukarudi juu na ku-loop. Golini Gabriel almanusra auokoe ila ukamchuna kichwa kidogo na kuingia wavuni. Bahati juu ya bahati.
Nakumbuka pia goli la Saka lilitokea nje ya box. Hata shangilia yake ya kukimbilia corner flag kuweka kidole kichwani, aliifanya kumjibu Rashidi ambaye awali alishangilia hivyo goli lake.
Naona hizi takwimu zinatuonyesha tu kuwa sisi tulikuwa hodari Kwa kutawala mashambilizi na yalitufikisha sana ndani ya box ila nyie mlikuwa vizuri kuyazuia na kupona chupu chupu. Nyie hamkutawala sana mashambuilizi hivyo hamkuingia sana ndani ya box ila mlipata magoli mawili mazuri sana ya kubahatisha.