Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Lawama zetu zimetoakana na kutumia vibaya mipira michache aliyopata sio kutopata mipira.
Na vile-vile hajitumi - work rate yake leo ni ndogo, tulimzowea tunapopoteza possession huwa anarudi kusaidia difensi kama anavyofanya Gervinho ama RVP, lakini yeye sasa naona kaamua staili ya Bendtner just anangoja mpira uje kwake hakuna ile team work
 
Huyu Gervinho kule France walikuwa wanamuachia anatembea na mpira mpaka goli, lazima ajue uingereza tofauti ana abadilisha style yake la sivyo atapata tabu sana.
 
Am sure we will go through from these UDINESE..... But then we never deserved this 1-0 result.....
 
Kwa kweli msimu huu kazi tunayo, tatizo AW na kamsemo kake "in Arsene We trusT" kanakua kananitia nguvu. Ila wakubwa, kama hatutasonga mbele sitashangaa!

Anyway usiku mwema, na ka goli kamoja, tutafanya nini?! Ndio AW wetu huyo!
 
Ni rahisi kuona Chamakh hafanyi kitu, lakini ukiangalia vizuri utagundua kwamba hakuna mipira inyofika kwake kutoka kwa viungo, pasi ya mwisho hakuna au mbovu!

Mkuu unauhakika tulikuwa tunaangalia match moja wote!!....

chamakh hakufanya lolote!!! leo hii! sawa mipira haifiki hata kuifuata basi...
 
kwa kweli msimu huu kazi tunayo, tatizo aw na kamsemo kake "in asrsene we trust" kanakua kananitia nguvu. Ila wakubwa, kama hatutasonga mbele sitashangaa!

Anyway usiku mwema, na ka goli kamoja, tutafanya nini?! Ndio aw wetu huyo!

mkuu kuna watu walidhani hatutashinda hii game!! Hahahahahaha!!!
 
What matters now ni kwamba tuna mechi ya marudio kule mjini Udine. Wachezaji Johan Djourou , Kieran Gibbs wameumia na kuna posibility Thomas Rosicky nae ameumia msuli.

article-0-0D744FD900000578-18_634x418.jpg

Theo Walcott akishangilia na Gervinho baada ya kufunga goli pekee dakika ya 4.

Theo_Walcott_1973594c.jpg

Liverpool, karibuni Emirates.
 
hongeri majirani kwa ushindi. jitahidini wiki ijayo maana kule channel 5sio kuzuri sana japokuwa mna nafasi ya kuchukua kale kakombe.
 
Bado tunaninginia kwenye tawi lakini kwa kamba ya mgomba na sio katani, muhimu tumepata clean sheet, na mechi ya marudiano Mungu atasaidia pengine Wilshere, Capitanyo RVP na pengine Nasri ( you never know) watacheza na Professa atakaa kwenye benchi - kibarua msimu huu ni kizito sana, lakini ni cha kujitakia wenyewe, tulifanya uzembe tukamaliza nafasi ya nne, tulifanya uzembe katika usajili na tunaendelea kufanya uzembe kutegemea wachezaji wasio na uzoefu.
Lini shilingi itadondoka kwa mabeberu (Arsenal board of Directors) Nahisi wanasubiri mapinduzi - Egyptian style.
 
Kabisa mkuu, bado ninamatumaini kwa Wenger labda atatushushia wachezaji kabla ya 08/31. Mungu ampe moyo wa kufanya maamuzi mazuri ya kuwapa furaha fans na sio board.
 
Kwa kweli jinsi vijana wanavyocheza, hakuna matumaini kabisa msimu huu!
 
Back
Top Bottom