Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Ila Arsenal daah still bado hata kocha yetu ana lack of maturity, kuna haja ya kula pindi kwa Fergie na Morinho ambao wanajua jinsi ya kucheza mechi za mwisho ambazo zina amua ubingwa.

Wachezaji nao inabidi wakue kidogo wajue tupo kwenye mbio za kugombea ubingwa, mechi ya pili tunaongoza mbili zote zinachomolewa.

Hivi Etihad hapo sijui itakuwaje daah.
 
Uliwaonya wadogo zako wakashupaza shingo
 
Usiogope mkuu hapo hamis anakwambia city hatakufa goal nyingi tu msiwe na wasiwasi.
 
To be honest siku ya leo nimeumia sana, sijajua kwanini coach anakuwa muoga kufanya maamuzi magumu. Kiuhalisia wachezaji kama Saka, Holding na Partey hawakuwa na form nzuri leo toka dk ya 1. Ilitakiwa uthubutu wa kuwafanyia sub hawa; nadhani White asiporudi kati ASAP in absence of Saliba basi kuna hatihati ya kutopata ushindi katika match hadi 4 zilizosalia vs Chelsea, City, Newcastle na Brighton.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu tumo humu since way back Emery anakua appointed.

Way back game ya kwanza ya Arteta Saka ni beki.

Way back tunaambiwa beki ya Arsenal haifundishiki.

Hapa tulipo siyo bahati mbaya. This is not overnight success.

So nyinyi mnaodai mlitaka Arsenal achukue nyinyi ni side quest tu mmechotwa na hiki mnachokiona. Hamuwezi jitamba kwamba uwepo wenu utaanua Arsenal achukue ubingwa ama la
 
Usiogope mkuu hapo hamis anakwambia city hatakufa goal nyingi tu msiwe na wasiwasi.
Daah mechi zao tatu za mwisho nimeziona City hawana masihala hata kidogo,kama jana ndani yadk 25 washamaliza mchezo.

Wale jamaa labda droo ushindi ni asilimia chache sana arsenal kushinda.
 
Angalia game yetu ya msimu uliopita dhidi ya Totenham (ya kuamua kwenda UEFA). Holding limeingia limepanick, tukafa.

Angalia game yetu dhidi ya City ya FA. Arteta anaweka rotation ya kisenge, tukapigwa. Angalia game yetu nyingine na City msimu huu Epl, Tomiyasu kapanic, wachezaji wanapoteza concentration, game tumepoteza.

Angalia Ueropa dhidi ya sporting cp. Ile first game tu inakuonyesha Ile ni timu ya namna gani, second match Arteta anafanya makosa yaleyale (rotation za kiduanzi, mechi za pressure kubwa), matokeo yake tumetolewa.

Na huu ubingwa tunaukosa Kwa makosa yaleyale ya miaka (kupaniki na kupoteza concentration)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…