Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,719
- 25,854
Xhaka hucheza uzuri akiwa na Partey kwani hupanda juu akiwa CM kusaidia mashambulizi na Odegaard, na Partey kuwa alinda back four na kuharibu mcheze wa timu pinzani.Pale kwa Xhaka panamshinda sikuiz, panamfaa zaid Fabio,
Kuna jamaa mmja humu aliwahi kusema Xhaka anacheza vizuri ila sio mnyumbulifu kama tukipata kiungo mnyumbulifu zaid Eneo lake tutakua bora zaid na zaid,
Kama Patey hayupo Xhaka hupata shida kwani yabidi kubakia pale katikati na hivyo Arsenal kushindwa kufanya mashambulizi ya mpangilio.
Timu kama Man City waliweza kuizidi sehemu ya kiungo ya Arsenal kwa kila kitu lakini Aston Villa ilikuwa ni 50-50 hivyo imesaidia kidogo Arsenal.
Xhaka ni mchezaji mzuri lakini tukumbuke first 11 ya Arsenal ni Martinelli pekee ambae angalau amepata wa kumpumzisha (Trossard) ila wengi wao akiwemo Saka wahitaji kupumzika baadhi ya mechi huko mbele.
Saka ndo hana wa kumbadili maana Nicolas Pepe hayupo, hivyo hata ikitokea apigwa viatu sana hujitahidi kuendelea kucheza game na kuugulia maumivu baadae.
Hiyo ndiyo Arsenal ya sasa ambayo yanikumbusha Arsenal ya 2004.
Kama tunavyoamini washabiki sasa Arsenal ubingwa ni wetu kuupoteza njia imesafishwa na Manchester City na tuna game in hand.