Kazi ya Potter hiyo. Kaijenga timu hata bila Caicedo na Trossard bado timu inacheza kibingwa
Mkuu Acha kumpakulia kocha wako Minyama ambayo haistahili...! Hiyo ni kazi ya Roberto De Zerbi mwenyewe
Potter kaondoka Brighton na ikapoteza michezo mitatu Kati ya minne, maana yake ni kwamba wakati anaondoka potter aliondoka na kila kitu chake
Potter ameenda Chelsea hakupoteza mechi katika michezo karibia 9 ya ligi kuu pamoja na UEFA ila akaja kupoteza alipokutana na team ambayo imepoteza michezo mitatu Kati ya minne ambayo ni Brighton
Roberto De Zerbi alijitafuta kipindi anapigwa back to back hadi akajipata na ndio tukaona hiyo team, ingekuwa Zerbi anatembelea Nyota ya potter basi asingepigwa kama Ngoma baada ya Graham kwenda Chelsea
Matokeo ni kwamba tunaweza kusema Potter ndio alikuwa anatembelea upepo wa Tuchel ndomana mwanzo Chelsea ikaonekana iko njema na baada ya kuanza kuipriment mbinu zake maji yakazidi unga ndio hadi leo
De Zerbi amekuta potter anamtegemea Moises na Trossad ila yeye kaja katengeneza team ambayo ata akosekane mchezaji muhimu bado inakupa matokeo
Trossard hakucheza hakucheza game 5 kutokana na matatizo ya kinidhamu ila Brighton ikaendelea kuwa yamoto kama kawaida, Mc Allister akakosa game 3 alipotoka world cup ila Moto ukawa ule ule
Subiri Potter atengeneze team nzuri hapo Chelsea tutampa tu sifa zake na sio kuanza kupewa sifa ambazo hazimuhusu, kwa sasa Brighton ilivo ni mipango ya Zerbi only