Nimeshangazwa na watu wanaodai Tierney auzwe July na wakiona White ni right back. Ben White alianza RB msimu huu kwa emergence tulikuwa nayo ya Tomiyasu kuwa majeruhi. Ben White ni CB na DM mwenye uwezo wa kuperform RB.
Tierney bado ni mchezaji muhumi katika timu na kwa miaka yote tumekuwa tukililia "Deep Squad", kikosi imara na bora kinakuwa na wachezaji wasiopishana uwezo sana na kwa kila nafasi.
Tomiyasu + New RB
Saliba + White
Gabriel + Kiwior
Zinchenko + Tierney
Tuungane kuwapiga vita wanaotaka kuona Tierney akiuzwa. Katika Msimu kuna mashindano manne lazima uwekeze katika deep 2 squad kuweza kushindana.
Ndugu hivi unadhani watu wanasema auzwe au Ni mahitaji ya timu yatamfanya auzwe?
Tierney kwa uwezo wake hawezi kuendelea kusugua benchi
Kumbuka Zinny na Tomiyasu Ni First priority linapokuja Swala la LB kwa Arsenal inavyocheza Sasa, hata KT mwenyewe alisema ana struggle kucheza hii role ya LB kuwa holding MD tofauti na Zinchenko au Tomiyasu ambao walishawahi kucheza hizo nafasi za Kiungo .
So huoni Kama Tierney kukaa bench na kuwa mchezaji wa Cups itamfanya aangalie sehemu nyingine?
Kumbuka Hata RB ambayo White amekuwa akicheza Bado Arteta anataka kuleta complete Inverted RB ,
Na bahati mbaya au nzuri Tomiyasu Bado anaweza kucheza hiyo RB , Kwahiyo White ana advantage ya katumika RB na CB mwalimu akimuhitaji .
Sio mashabiki wanataka auzwe ,ila nafasi ya KT kucheza imekuwa finyu ,hasa Baada ya Arteta kuacha kutumia LB Kama winger ,
Juzi hapa alitoka Martinel akaingia KT Kama winger ,na sio LB , hiyo Ni ishara taratibu Arteta anaachana na KT Kama LB Labda itokee Zinny na Tomiyasu injury ndio unamuona KT akipata nafasi LB ,
Zaidi ya hapo asubiri FA cup au Carabao ,
Hapo lazima atatafuta maisha kwingine , Labda Kama asiwe na tamaa Sana ya kuondoka.