Ndg wana gunners
Kwa heshima na tahadhima napenda kutoa PONGEZI za dhati sana kwa klabu ya Arsenal na mashabiki wake wote na sera yake ile pendwa ya kutoingia kwenye bidding war na timu zingine wakati wa kumnunua mchezaji. Hiyo sera sisi Chelsea tumekuwa wanufaika wakubwa sana na tunaomba kwa mwenyezi Mungu hiyo sera idumu milele na milele.
Jana mlimuona kijana anawatapisha Nyongo akina Milner, Gomez na wenzake. Hata akina Galagher na Chunkuemeka kidogo watapishwe nyongo kwa sababu ya pasi za haraka haraka.
Huyu dogo amekuja kutuondolea ubishi tuliokuwa nao kwamba eti tuna wachezaji class.
Sasa hata pasi za Mudryk hawawezi kupokea, ni Ziyech tu naona wataendana naye.
Kwa hiyo tunatangaza rasmi sasa Ziyech not for sale.
Ujenzi huu wa timu sasa utajengwa chini ya msingi ambaye ni Mudryk, the next Messi and Chelsea Messiah.
Tukimaliza kumsajili RB na viungo wawili, tutazindua rasmi Chelsea kurudi kwenye ligi, sasa hivi tumewaachia tu turekebisha masuala yetu ya ndani.
Kwa heshima nyingi narudia tena kusema asanteni sana majirani zetu, mlichokifanya hakitasahaulika pale darajani.
London is Blues and Blue forever.