Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Daaahh HENRY14 nimejitahidi sana kufatilia comments zako na nimejihakikishia bila ya shaka yoyote kua wewe ni mpenzi halisi wa mpira na wala sio shabiki wa mpira kama kina sisi.
Comnents zako nyingi hua unakua muwazi sana pasi na kuingiza unazi na ushabiki wa timu unayoishangilia.
Hongera sana mkuu HENRY14 akina sisi hua tunajitahidi kua kama wewe lakini mara nyingi mahaba ya timu tunazozishabikia hua yanatutoa kwenye reli.
 
Hua nashangaa timu kama Napoli au Dortmund wanaingia chimbo wanakuletea mtu wa 16M na anawasha moto mpaka chelsea et el watakuja kutoa 100M

Kwamba Arsenal scouting yetu haina connection sana au?
Add Brighton hapo kwq siku za hivi karibuni.

Angalia wale wakina Mitoma ,Caicedo hata 10 haifiki ila sasa hivi ukimtaka hata mmoja sio chini ya 60M
 
Last year hatukusajili forward tukapiga kelele top 4 ikasepa kama utani and now on naona yale yale yanajirudia tena 11 squad ya kutisha but benchi hoi bin taabani anyway let's wait and see
Dah mara 10 tungemchukua Felix kwa mkopo kuliko kukosa vyote inaweza kutucost sio tu ubingwa especially Akiumia Saka ama Martinelli.
 
Last year hatukusajili forward tukapiga kelele top 4 ikasepa kama utani and now on naona yale yale yanajirudia tena 11 squad ya kutisha but benchi hoi bin taabani anyway let's wait and see
Kabisa aisee, tuna delay sana kwenye deal moja, alf ndo kama hiki kilichotokea mpaka sasa tungekua tumekamilisha sajili mbili fasta kuongeza nguvu kikosini, au hadi tufungwe ndo watakumbushwa,..
Alf ukisema watu watakuja kudai usajili ni mchakato, mbona timu zingine siku tatu ama nne deal done. Sie wiki 3
 
Dah mara 10 tungemchukua Felix kwa mkopo kuliko kukosa vyote inaweza kutucost sio tu ubingwa especially Akiumia Saka ama Martinelli.
Ngoja tuone labda kuna best option zingine zipo, nahis saiv Edu na wenzake watakua wameamka kuhusu kuchelewesha deal, kama timu haieleweki kukuuzia mchezaj achana nao basi
 
Hakuna cha mchakato wala nini that's is stupid excuse tuna squad yenye nguvu ila benchi la kifala na tuseme kuwa hao 11 players watacheza bila injuries up to June haiwezekani last year top 4 ilikosekanika sababu ya haya haya
 
Aaron Arsenal yuko wapi na simulizi zake za mudryk
Aaron Arsenal kakimbizwa hospitali presha ilishuka ghafla akadondoka chini na kupoteza fahamu, kilichompata Manara Dubai kwa mke wake wa pili ndio hichohicho kimempata ndugu yetu Aaron Arsenal kwa Mudryk, kikubwa tumuombee tu dua apone haraka ila mtihani anaoupitia ni mzito sana tusitegemee kumuona humu ndani ya kipindi kifupi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…