Sijui kwanini watu wanawachukulia Liverpool kiwepesi, labda sababu wapo 10th, binafsi naona mechi yetu dhidi ya Spurs hata kabla ya red card ilikuwa nyepesi kuliko mechi dhidi ya Liverpool. Mechi dhidi ya liverpool ilikuwa ON hadi dakika ya mwisho.
Kitu ambacho Klopp alistruggle dhidi ya Arsenal ni utengenezaji wa nafasi, liverpool walirecord the least XG ndani ya misimu miwili, forward hawakuwa na tatizo kwenye finishing, nafasi nyingi walitengeza kutoka deep lengo lilikuwa kuexploit Arsenal's high line kwa kumtegemea TAA/ henderson, baada ya kutoka TAA approach ya Mikel ilibadilika akajiamini zaidi kushambulia. So Liverpool si wepesi sababu wamefungwa na Arsenal, Liverpool si wepesi km Ollachuga unavyotuaminisha, wakiwa fully fit utahitaji kuwa organized mwanzo hadi mwisho ili kuwafunga.
Kama shabiki wa Liverpool unaiona hii Liverpool ni mbovu basi ujue tu Arsenal tushacheza Anfield na backline ya Sokratis, Bellerin, Mustafi, lichsteiner mzee kutoka Juve, kocha akiwa Unai emery, midfield kuna Guendouz, LT11, foward tukiwa na lacazette, benchi yupo Joe willock , Firmino anafinya anavyojisikia, Mo Salah anapiga anavyojisikia, ilikuwa inatia uchungu sana.