PRE-MATCH ANALYSIS: Arsenal Vs Liverpool
Faida ya Liverpool itakua sehemu mbili. KWANZA kucheza Long balls na ku-win second balls. Wanawachezaji wanaoweza kucheza long balls tena kwa kiwango kikubwa. Allison, TAA, VVD, Robertson na wengine ni wazuri wa kunzisha Long balls.
Kwa sababu ya physicality (Uwezo wa kutumia nguvu) ni vyepesi sana ku-win (Kushinda) second balls. Hapa namzungumzia Henderson, Fabinho, Darwin Nunez, Salah dhidi ya Saliba, Gabriel, Partey
PILI ni kutengeneza 1v1 na kushambulia spaces (Eneo lililowazi) na kutengeneza mikimbio nyuma ya mabeki (Behind the Lines) japo kwenye 1v1 itakua ngumu sababu ya namna Arteta anavyofanya Overloads (Idadi ya wachezaji wengi)kuanzia safu ya ulinzi mpaka kiungo (Rejea Arsenal Vs Tottenham).
Kwasababu ya kupungua kwa uwezo na ubora wa kufanya Pressing na kuongeza Pressure kwa timu pinzani, Klopp na Liverpool wame-switch kutoka 4-3-3 kwenda 4-4-2 hivi karibuni (Rejea Vs Rangers UEFA) na inampa faida. Kivipi?
Kwenye Build up akiwa na 4-3-3 shape inabadilika kwenda 2-3-5. Wings zote (Diaz na Salah) wanafanya pressing kwa kuingia ndani na kua sambamba na Centre-backs wa timu pinzani huku Full backs wake akiwemo TAA na Robertson/Tsimikas wakifanya pressing kwa Fullbacks kwa timu pinzani na kufanya idadi kwenye wachezaji kwenye mashambulizi kua 5 akiwemo #9’s (Firminho/Nunez/Jota).
Ukirejea kwenye game Vs United wakiwa wanafanya Build Up na kufika kwenye Final Third, kwenye eneo la kiungo wanaacha space sana ambayo ni rahisi kuadhibiwa. Kwenye box la United kulikua na Diaz, Milner, Firminho, Salah na Hernderson kiasi cha kuacha Space katikati Kwa Eriksen/Fernandez kufanya mikimbio. Hivyo Klopp kurudi kwa 4-4-2 kunampa faida kwasabau hatoacha spaces kwenye Build Up.
Kama ilivyo ada kwa Arsenal, kutengeneza 3-2-4-1 (Au 3-2-5) kwenye Build up itapunguza speed ya kushambulia kwa Liverpool kwa namna gani?…
Saka na Martinelli wanapanua uwanja kwa juu zaidi na kufanya TAA na Robertson/Tsimikas kutokupanda na kutoa pressure kwa Zinny/Tieney na White (Full backs wa Arsenal) ambapo Jesus akifanya Pressing katikati ya mabeki wa kati wa Liverpool (VVD na Matip) hali ikayowafanya kutegemea Long balls na kushinda second balls.
Katikati ya uwanja Partey na Zinchenko/Tierney huku kwa juu yao Ødegaard ambapo anatapa cover ya Jesus (Aki-link na midfield) ambapo atamuacha Xhaka free na uwezekano wa kushambulia kupitia nafasi za wazi (Space) inakua kubwa. Partey anakua kama Scanner (Rejea Vs Spurs) na kazi yake kubwa ni kusimama juu ya mstari wa mabeki wa nyuma (Saliba,White na Gabriel) na kufanya block na interceptions. Uwepo wa Partey unapunguza 1v1 na kufanya idadi ya wachezaji kua wengi (Numerical advantage).
Kwakua Salah na Diaz ni wazuri kwenye 1v1, itakua hatari kama Arsenal na Arteta ako Acha hivi ndio maana anatengeneza uwepo wa Partey na kutengeneza 5v4 wa Liverpool (Yaani White, Saliba, Gabriel, Partey na Zinny/Tierney dhidi ya Diaz, Jota/Firminho, Henderson na Salah) huku TAA na Roberson/Tsimikas wakiwa pinned back (kuzuiwa wasishambulie) dhidi ya Saka na Martinelli.