SIRI ZINAZOMPA ARTETA USHINDI ARSENAL
1: Football Brain
Kwenye Football,kama Kuna kitu kinachowasaidia makocha wengi kufanya Kazi vizuri na kwa wepesi sana ni Football Brain.
Football Brain inamsaidia kocha kuona mambo mengi sana ndani na nje ya uwanja,hiki kitu kinamsaidia kocha kujua kila mchezaji anacheza kwa intensity gani,anakuwa vyema akiwa wapi,ni mzuri kwenye maeneo gani, ni mzuri kwenye mipira gani na anafurahi kufanya nini uwanjani.Hadi Leo toka Arteta afike Arsenal Mchezaji pekee ambaye uwezo haukuongozeka ni Pepe tu ambaye nae Leo hii hayupo Arsenal lakini nyote ni shuhuda wa hiki anachofanya Xhaka,Saliba,Gab wote,Saka NK.
2: System
Arteta amefanikiwa kutengeneza system ambayo Leo hii imefika sehemu unaweza usione gap la mtu kwenye vile vitu basic vya uchezaji japo utakosa vitu vichache sana ambavyo ni individuals.Kwenye system aliyotengeneza Arteta anaingia mchezaji yeyote na anafanya vizuri na team inaendelea na flow ileile hata asipokuwa na wachezaji waliozoeleka.
3: Spirit ya Team
Hili kocha ufanikiwe kwenye mpira unahitaji kuwa na team ambayo itakupigania Wewe kama kocha,itaipigania nembo ya team Yao kwa jasho lote.Arsenal ya Arteta inacheza kwa ajili ya Arteta , inacheza kwa ajili ya Arsenal .Ametengeneza team ambayo haitaki kufungwa mechi ,team ambayo inapigana muda wote kuutawala mchezo ndo maana unaona Arsenal wako pale walipo Leo wanachokiwaza ni kushinda mechi tu na sio kitu kingine.
4: Versetility
Kwenye mpira kocha mwenye akili lazima atakuwa na akili ya Ziada ambayo itamlinda,akili hii inaenda mbali na Kuna muda Huwa inaziacha mbinu husika za mwalimu.Arsenal ya Arteta Ina wachezaji zaidi ya 6 ambao wanaweza kucheza position zaidi ya Moja na Hilo ndo limewasaidia kufika apo walipo,Kuna muda zile spinal cord za team zinaumia na kukosekana kwenye michezo kadhaa lakini bado Kuna watu wanaingia kujaza zile nafasi na wanafukia mashimo Yale na kuirudisha team kwenye stability ya uchezaji. Hii ni Moja ya siraha ambazo zimembeba Arteta kwa kiasi kikubwa hadi sasa.
5:Back staff
Kuna vitu wenda wengi bado wanajiuliza inawezekana vipi arsenal wanacheza Vizuri vile na kushinda mechi kiwepesi lakini jibu ni Moja tu hapa (Back staff).ukiachilia mbali Ile exploration talent ID ambayo Arteta anayo Ila kwenye benchi amezungukwa na watu makini sana ambao wanampa back up kubwa kwenye utekelezaji wa Majukumu yake.Tulizoea Arsenal kufungwa goli aina Moja lkn Leo hii Kuna muda unawaza watafungwa vipi jibu hupati ...hii back staff ya (Set pieces coach,Technical analyst,GK coaches) ndo turufu inayofanya Arsenal ya Arteta ifike apo bila shida.
6:Ndoto
Hii inaweza kukushangaza lakini unatakiwa utambue kuwa Arsenal ndo team yenye avarage ya umri wa miaka 23 kwenye ligi Tano Bora Ulaya.Kwa umri huu wachezaji wengi walitakiwa wawe wanacheza mechi za academy Lakini wapo Arsenal wanacheza ligi kuu.Huu ni umri ambao mchezaji Huwa anaota kutengeneza rekodi nyingi nzuri,anaota kufanikiwa kwenye career yake,anaota kufanya makumbwa na kuwa mtu mkubwa.Hiki ndo kinafanya Ile team icheze kwa moyo mmoja kwasababu Wana ndoto inayofanana.
NB:
1-Hii timu inaweza isipate mafanikio msimu huu lakini ndani ya misimu miwili mbele itabeba makombe.
Naitwa #Ramsey
View attachment 2372889