ARTETA ALIMFUKUZA AUBAMAYANG LICHA YA VIONGOZ WA ARSENAL KUMTETEA
Mikel Arteta alikusanya ripoti ya makosa ya Pierre-Emerick Aubameyang kabla ya kumfukuza mshambuliaji huyo kwenye kikosi chake cha kwanza - akipinga shinikizo kutoka kwa wakuu wa Arsenal kumuomba asimuache.
Meneja wa Arsenal alitoa maelezo ya kina kuhusu matukio hayo, ikiwa ni pamoja na nyakati na tarehe, akijenga ushahidi kabla ya kumwachisha Aubameyang na kumvua unahodha kwa makosa mengi ya kinidhamu Desemba mwaka jana.
Arteta hakukata tamaa, licha ya Edu, mkurugenzi wa ufundi wa Arsenal, kumtaka ampe nafasi Aubameyang tena, na klabu hiyo ikakatisha mkataba wake wenye thamani ya pauni 350,000 kwa wiki, kwa kumlipa takriban pauni milioni 7 kabla ya kujiunga na Barcelona kama mchezaji huru.
Source:The Times UK