Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Waleteeee
 

Attachments

  • IMG_20220805_123318.jpg
    IMG_20220805_123318.jpg
    350.4 KB · Views: 12
Kwa hiyo waliotoa hiyo pesa ni wajinga? Mbona huyo huyo Pep aliuziwa Grealish kwa paundi million 100! Hakuna unachojua kuhusu hizi biashara na kila usajili ni kamari. Ukilielewa hilo wala hautaumiza kichwa
Angalau Jack tayari alikuwa na misimu kadhaa kafanya vzr Aston Villa
Sasa huyu cucu msimu mmoja TU tena best performance yake Ni ile mech na man u
 
Arsenal fc inafanana na yule mbwa mkali kwao (Pre-season), mpaka wanafamilia wanampa jina la Simbaaa.

Lakini simbaaa akipelekwa josho kuoshwa, akikutana huko na mbwa wa polisi (EPL), simbaa anaficha mkia matakoni, analala chini, anavutwa hataki kwenda.
Zile 4-0 ,6-0 za preseason zinawauma

Mbona mwaka jana preseason tulianza ovyo ,Hadi mkatupiga 2-0

Safari hii tumewagonga 4-0 na mpira mwingi

Mmeanza mchecheto ,tulieni muone Sex football

Nyie komaeni kusajiri mabeki
 
Kirafiki wakati wahezaji was Chelsea wanakwambia ile sio friend match

Gorginho anasema kabla ya mech wanaenda KUPAMBANIA wewe unadai waliachia
Sina maana waliachia. Nilitaka kumaanisha haikua mechi ya kubeba attention kubwa ya wachezaji kama ilivyo kwa ligi kuu au mechi ya mashindano umuhimu ulikua ni kutafuta fitness
 
Angalau Jack tayari alikuwa na misimu kadhaa kafanya vzr Aston Villa
Sasa huyu cucu msimu mmoja TU tena best performance yake Ni ile mech na man u
Unamuongelea hapo mchezaji aliyeshinda player of the season ndani ya huo mwaka wake wa kwanza. Put some respect on his name
Screenshot_20220805-140429_1659697497664.jpg
 
Ile ilikuwa ni preseason mlidhani ligi yenyewe haitafikaaa 😀 😀 😀 leo mkifa chache ni 2
Leo wanaenda kuliwa kimasihara na wahuni wa palace, kisha watakuja kwenye ule uzi wetu pendwa kuelezea jinsi walivyogongwa goli 3 kimasihara kwa ile style mpya ya mtumbwi wa vibwego.
 
Chelsea ni timu mfu, ndio maana wachezaji wanaikataa.

Acha kuiweka kwenye kundi la timu za maana.
Unavyosema wachezaji wanatukataa sijakuelewa kwasababu koulibaly, sterling, Cucurella wamekuja kwetu na frenkie de jong katuchagua over man u
 
KILA LA KHERI TIMU YETU ARSENAL DHIDI YA PALACE

Mechi ya mwisho tulifungwa 3-0

Patrick Vieira aliwatarget Full backs zetu, NUNO NA CEDRIC ,aliwapress Sana akimtumia Zaha na Ayew , akabaki Partey akaumizwa, mech ikawa yao .

Na sote Tunajua ukiwapress Nuno na Cedric Ni majanga hutokea,

Leo hakutakuwa na Nuno Wala Cedric

Leo tutarudi na kikos kile alichopigwa 6-0 Sevilla ,4 -0 CHELSEA

Saliba ,Ben White na Zinny wapo njema Sana na mpira mguuni ,

NATARAJIA MABADILIKO MAKUBWA KIUCHEZAJI, LAKINI PIA TUWE MAKINI NA KAUNTA ,MAANA WATAWATUMIA ZAHA NA EBOWEI AU ZAHA NA EZE

Leo watamkosa Olise ,pia hawatakuwa na Gallagher ambaye amerudi Chelsea.
Ila msije baadae kuanza kumlalamikia kocha
 
Lucas Torreira will sign the contract as new Galatasaray player today. Meeting already scheduled in Italy in order to get it over the line as soon as possible. 🚨🟡🔴 #Galatasaray

Arsenal have already prepared all the documents to be signed for €6/7m deal. https://t.co/vW0wLKNJYV
 
Mamluki kutoka majukwaa mbalimbali kuja humu kwetu kupiga domo inamaanisha wanatishwa sana na msimu tutakaokuwa nao mwaka huu.

Najua wapenzi wote wa mpira duniani ikiwemo vijana, watoto na bila ya kuwasahau wazee, watafika mapema kwenye runinga zao na vibanda umiza kushuhudia soka safi kutoka kwa timu yenye vijana wenye uwezo zaidi ndani ya EPL.

Nawaahidi hatutawaangusha, soka safi litatandazwa kwenye kapeti na damu changa tulizonazo.

Wa kukosoa mjiandae.. na wale mtakaoleta tabiri zenu baada ya mechi ya kuwa hatutofika mbali pia tunawasubiri.

🔴⚪#COYG💪
 
Back
Top Bottom