Kacheza mechi ngapi ana magoli mangapi?mimi namkubali huyu jamaa,
Kacheza mechi ngapi ana magoli mangapi?mimi namkubali huyu jamaa,
msimu huu alianza vzr tu, akaumia ,Kacheza mechi ngapi ana magoli mangapi?
Alinunuliwa mpunga mrefu ila sasa hivi siyo regular startermsimu huu alianza vzr tu, akaumia ,
View attachment 2129122
Spurs ni kichekesho.
Uwepo wa michuano kama FA na Carabao ni kwaajili ya kujaribu combinations pia.NINAJARIBIWA KUWACHEZESHA WOTE KWA PAMOJA(SMITH,MARTINEL,SAKA,ODEGAARD)
Mikel Arteta anajaribiwa na wazo la kuwapanga nyota wote wanne washambuliaji wa Arsenal - Bukayo Saka, Emile Smith Rowe, Gabriel Martinelli na Martin Odegaard - kama sehemu ya safu mpya ya Ushambuliaji.
Kufikia sasa msimu huu, Arteta amekuwa akimuacha mmoja kati ya hao vijana wa nne na badala yake Alexandre Lacazette ameongoza safu hiyo.
Lakini sasa Arteta ana umiza kichwa kwenye kuchagua kwani Martinelli amerejea kutokana na kusimamishwa dhidi ya Wolves na, kabla ya kadi yake nyekundu, fomu ya Mbrazil huyo ilihitaji nafasi ya kuanza.
Martinelli, Odegaard, Saka na Smith Rowe kwa pamoja wana wastani wa umri wa miaka 21, lakini Mhispania huyo amekiri kwamba hili ni jaribu.
"Wamecheza pamoja - Emile alicheza kama kiungo mshambuliaji wa kushoto, ambayo ni nafasi nyingine ambayo anaweza kucheza," alisema
"Nimejaribiwa, ndio, kwa sababu wanataka kucheza na unapoona wachezaji wakifanya mazoezi na kucheza jinsi wanavyofanya, unataka kuwatupa wote uwanjani. Kwa bahati mbaya, wanatakiwa wachezaji 11 tu.
Ili kuwaweka wote wanne, mmoja wao angehitaji kuongoza safu ya ushambuliaji na Arteta anaamini Martinelli au Smith Rowe wanaweza kufanya hivyo.
"Inategemea na jukumu unalotaka wacheze na jukumu unalotaka kutoka kwa wale tisa," alieleza.
"Wana sifa tofauti sana, wangebadilisha mfumo wetu na nafasi(HALF SPACE ) ambazo tungeshambulia,..........
"Ingetegemea aina ya mpinzani pia, kuelewa ni muktadha gani ungewanufaisha wote wanne.
"Wamebadilishwa nafasi nyingi pia na lazima tuwe waangalifu wakati mwingine na jinsi tunavyowabadilisha. Lakini wanapokuwa tayari, ni fursa nyingine ya kuwatumia pia katika siku zijazo.”
View attachment 2129135
nadhan ndicho anachowaza arteta, amemuongelea na laca, hiyo comb ni next season labdaUwepo wa michuano kama FA na Carabao ni kwaajili ya kujaribu combinations pia.
Sasa hivi kwenye ligi hauwezi test kwakua waweza kuta mpaka dakika ya 70 matokeo hayaeleweki hivyo inabidi majaribio yasubiri.
Kichwani kwangu naona kama vile hii combination hata siyo mbaya, tuanze kama kawaida na Laca, dakika za 60 toa Laca, Martinelli awe CF aingie Emile akae namba ya Martinelli kisha observe.
Martinelli alishakua CF na alizitendea sana haki krosi za Tierney.

Sina wasiwasi kabisa.Mijadala inayoendelea humu, ni wazi jinsi gani utimamu wa hili jukwaa na umakini wa watu wa humu
Nafarijika sana kuona sasa tunawachambua wachezaji wetu kiufundi na jinsi gani squad ya ushindi. Big up kwa mike arteta
The gunner forever, wadau msichoke kutupa nondo kama hizi na madini mengine mengi mengi
Much respect all the gunners
By any means tuingie top 4, tofauti na hapo vitu vingi vitafeli on the process
Nafasi 3 or 4,
Chelsea akijichanganya tunakaa sisi pale
spurs na hummers wameshajifia
Nyumbu hizi game za mwisho atatumia sana VAR na marefa kuliko wachezaji na genggeng pressing
Njia pekee hapo arsenal kila game inabid aondoke na 3
Haijalishi tumecheza mpira wa aina gani (eg arsenal vs Wolverhampton 2-1)
#COYG
Mechi za Arsenal sipendi na uwa siangalizii kwenye vibanda umiza. Nataka niwe sehemu ambapo nitasikia kila kitu kinachoongelewa, that is home.Kuangalia mpira vibanda umiza kuna raha yake.
Jamaa kabadilisha game kwenye TV mbili tofauti coz of sauti. Game ya Liverpool vs Leeds kapeleka kwenye TV yenye sauti kubwa na Atletico vs United akabadilisha akaweka kwenye TV yenye sauti ndogo.
Mshabiki anataka arudishiwe jero lake maana kuna TV haina magoli 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Kuwekwa tu kwenye TV yenye magoli Joao Felix karudi na bonge la goli.
Hahaahahahahahaahahahahah
Same to me bro.Mechi za Arsenal sipendi na uwa siangalizii kwenye vibanda umiza. Nataka niwe sehemu ambapo nitasikia kila kitu kinachoongelewa, that is home.
moja ya mbinu watakayokuja nayo Wolves I believe, is to provoke our players because they know some of them are temperamental. If they manage to control themselves then winning is imminent/Mechi ya leo inaweza kuwa ngumu sana kutoka na sababu kadhaa
1. Moja ni vita ya top 4 maana wolves nao wanaona kuwa kuingia top 4 inawezekana
2. Kwa yeyote atakaeshinda mechi ya leo anakuwa juu na anakuwa na mzingira mazuri
3. Mmoja(arsenal) atataka kuonyesha ukubwa wake na mwingine(wolves) kuonyesha kwamba mechi iliyopita ilikuwa bahati na wala sio uwezo.
Japo mechi inaweza kuwa ngumu lkn bado mimi naona Arsenal anayo nafasi kubwa ya kushinda hii mechi lbd km wolve watakuja na mbinu ya kulinda zaidi huku wakitegemea mashambulizi ya kushitukiza na bado sioni km inawaeza kuwabeba sana hasa ukitegemea defence ya arsenal imekuwa bora sana hivi karibuni na pia uwepo wa Xhaka na Partey kumeifanya timu kuwa imara zaidi