Wachezaji waliopata yellow card December ni Ramsdale, Odegaard, Partey, Saka, Xhaka, Gabriel, Martinelli na Holding.
FA inamchunguza mchezaji kwa ajili ya yellow yenye viashiria vya kubet. Inadaiwa kwamba anayechunguzwa ni Xhaka na yellow inayochunguzwa ni ile tuliyocheza na Leeds ambapo tukiwa tunaongoza 4 - 1 Xhaka akapata kadi kwa kupoteza muda.
Tuassume ni kweli kuna mchezaji kafanya hivyo. Mchezaji analipwa 100K+ kwa wiki unadhani ni kiasi gani kinatosha kumfanya ashiriki katika hii bet? Naamini inatakiwa iwe pesa nyingi kweli kweli maana hii ishu ikibumburuka na career yako inaweza ikawa ndiyo imeisha.
So let's hope siyo kweli and let's hope siyo Xhaka kwakua red tu zinafanya achukiwe na hili likiingia kwenye huo mchanganyiko itakua mwisho wake kimpira.