Kuna tofauti kubwa sana ya Mashabiki walioziea kuiona Arsenal ya Makombe na Wale waniaipenda wakiwa na upungufu wa mataji.
Ukiirejea rekodi toka sisi wa kitambo kidogo wakati epl hasa inaanza kuruka TZ miaka ya 97/98 Arsenal ilikuwa haichagui wa kufunga awe Manyua au Upupu (Fools) Nyukasto wakati huo wakiwa wa moto.
Hoja za anayesema Arsenal bado hatujapiga hatua ni kulingana na Matarajio ya kuiona inarejesha makali yake yaliyokoma 2005.
Kwa wanaosema imepiga Hatua reference yao ni uwezo wa kupambana na midtable team.
Kwa hoja hizo kila mmoja yupo sahihi.
1. Kuzifunga team ndogo na kusema tumepiga hatua ninsahihi - ila expectations ziko low. Hakuna mawazo ya kuchukua Ubingwa.
2. Kuzifunga team ndogo na kusema bado tunapiga marktime - expectation za U ingwa hizi, ndiko Arsenal inakotakiwa kurejea.
Mwisho wa siku Tukubali kutokukubakiana na huu unakuwa msingi wa Heshima Baina Yetu.
Jana nilikuwa naangalia mpira na Mwana hatufahamiani wote ni Arsenal, tulikuwa na mazungumzo mazuri hadi ilipofika Sub ya Elneny, mwana alimsifia Jamaa anapiga kazi chafu sana, jibu langu kwake lilikuwa Sioni improvement from Denilson... Then nikitukanwa na kuambiwa sijui mpira. I respected him na kuhama meza kuepusha shari kitoka kwenye matusi toka kwa mtu nisiyemfahamu.
My point is tujifunze kukubali kupingwa tunapowasilisha mada, maana kwenye kupingwa kama hujajengwa basi unawajenga wanaokupinga. Mwisho wa siku furaha inatawaka baina yenu.
Matusi ni sehemu ya frustration unaweza kuta mtu ana mambo yake binafsi yanamaonga bahati mbaya ukaingoa kwenye 18 anakumalizia hasiara zote. Tujifunze kufunzwa na wenzetu.
Tupingane kwa hoja na sio Matusi. Sisi ni wakomavu zaidi ya matusi yetu.