Ili mchezaji awe na mental strength & Leadership anahitaji kitu gani?
Kwa upande wangu ningejibu anahitaji vitu kadhaa na miongoni mwao ni
1.kujifunza kutokana na makosa anayofanya-kila kosa waga lina athari zake na mara nyingi waga ni athari hasi na kufatiwa na athari chanya, ukishakosea unaigharimu team hiyo ni athari hasi ila kutokana na hilo kosa utajifunza hiyo ni athari chanya, hapa Xhaka ni wazi kwamba hajawahi kujifunza kutokana na makosa yake, Gabriel amekosea ila tutaangalia baada ya kukosea je atajifunza
2. Maturity, mchezaji anaweza akawa mdogo kiumri ila amepevuka kiakili vya kutosha katika kutambua majukumu yake, anafanya vile vya ulazima tu na Kwa faida ya team hapa utaona wachezaji kama kina Foden,Saka au alivokuwaga Fabregas ktk umri mdogo nk, ila mchezaji anaweza kuwa mkubwa kiumri ila hana maturity
3. Experience, ni mara nyingi uzoefu kwenye utendaji wa shughuri yoyote ile huleta mabadiriko chanya tofauti na mtu ambae hana uzoefu, japokuwa kuna baadhi ya watu pamoja kuwa na uzoefu katika shughuri zao ila hawaoneshi kama wamekomaa
4. Na mwisho kabisa tukumbuke Readership imegawanyika, kuna ambao wao ni born ready (kipaji) Kwa ajili ya uongozi na ambao wao wanapitia stage flani flani ili wawe viongozi, ikiwemo uwezo wa kujifunza unapokosea, maturity na uzoefu ila Kwa ambao ni born ready ni kama walivo kina Fabregas
Sasa ukiangalia hizo sifa 1-3 tukiacha unafki na mapenzi upofu, Xhaka hajawahi kujifunza, Xhaka hajawahi kuwa matured pamoja na umri wake na kibaya zaidi hajawahi kuonesha kuwa yeye ni mchezaji experienced, ni kama vile ana homa za vpindi, kuna muda anafanya makosa ambayo alitakiwa afanye Lukonga coz guy is young, immature and inexperienced
unajua kuna muda Xhaka marefa wana mkondem kutokana na record yake mbovu ya nidhamu, kuna muda unaona kabisa kosa alilofanya Xhaka akapewa adhabu ila akifanya mchezaji mwingine adhabu zitakuwa tofauti, hiyo ameijenga yeye mwenyewe kutokana na kutokubali kubaridika,kujifunza na kupevuka