Angalau tutajadiliana ki-mpira.
Naomba ushahidi wa hili usio na shaka ndugu yangu, kwamba hao makocha hapo juu uliowataja walikataa kwa sababu ya mahitaji yao ya pesa. Kama huna hii itakuwa ni story tu za vijiweni.
Lukonga amesajiliwa kwa fedha, Guendouzi ameondolewa kwa mkopo (pengine tunalipa part ya salary), hili unadhani ni kosa la tajiri??
Ben White amesajiliwa kwa £50M, Saliba hakupewa hata nafasi ya game hata 1. Something is really fishy here bro, hili unadhani ni kosa la tajiri?? Why not use Saliba from the first place uende umsajili White???
Ninachokiona ni kwamba Edu na arteta wanapiga hela kimya kimya na nadhani tajiri ameshtuka juu ya hilo.
Madrid wanaenda kutupiga pesa za kutosha kwa odeegard ambae hatumuhitaji. Hahitajiki Odeegard, Arteta kwa chuki zake tu na udhaifu wake akamuondoa alie Bora Martinez na kumuacha Leno je hilo nalo ni kosa la tajiri?? Tukiangalia in the past five years miongoni mwa timu zilitowa peas nyingi kwa ajili ya usajili pale EPL utaikuta Arsenal IPO pengine ndani ya top 5. Tunamlaumuje tajiri hapo??
Kuna kocha tulihusishwa naye kabla ya Arteta ila sidhani kama hata alikua approached.
Hili la Saliba niliwahi lisema humu. Saliba na Fofana wametoka timu moja ambayo hiyo timu Saliba ni nahodha, kitakwimu Saliba kamuacha mbali Fofana na wa kwanza kuja EPL alikua Saliba.
Fofana amekuja ndani ya wiki mbili anagewa namba Leicester huku Arsenal wanasema Saliba hayupo tayari.
Kisha Saliba akarudi ligue 1. Mpaka ligi inaisha nafikiri hakuna aliyefanikiwa kumpita kwa kudribble.
Guendouz ana attitude nzuri. Shida yake ambayo kila siku naisema ni hana chochote kitakachomfanya awe starter day in day out, stamina hana, pace hana, skills hana, vision hana. Notice kwamba Emery kamtoa daraja la pili (au la tatu) Lokonga sijamuona akicheza ila stats zake zinaongea vizuri. Sidhani kama tumepotea kwa Lokonga.
White usajili wake ni wa kuziba pengo la Luiz ambaye kwa Arsenal alikua ndiye beki anayeweza piga long balls kuzidi waliokuwepo. Na White anaweza hizo long balls so usajili wake ni ule wa kutaka timu icheze kuanzia nyuma. (Maelezo siyo yangu)
50M is ridiculous but wote tunajua katika negotiation kuna vitu vinaangaliwa. Muda uliobaki katika mkataba, umri wa mchezaji na timu yake inamuonaje.
Odegaard kuanzia amekuja mpaka ameondoka ametengeneza nafasi nyingi kuzidi aliowakuta lakini kiukweli mi naona Odegaard ni mchezaji ambaye hakufanya nilichotarajia. Ama hivyo au kocha hajui jinsi ya kuextract potential ya mchezaji skilled kama yule.
So kwangu ni mchezaji ambaye ni bora aje tena ila kwa mkopo na option ya kununua iwepo ikatokea kuna vitu ametimiza.
Tuna Leno. Tumemaliza msimu timu ya tatu kufungwa magoli machache. Tuliowauzia Martinez wako wapi? Varane kwa pesa aliyouzwa imeonekana Madrid ni wajinga lakini wangekaza shingo angeondoka free kama Ramos na kama donnaruma. Na sisi yangetukuta. Martinez anahitaji kua starting XI ili apate namba Argentina.
Sidhani kama Arsenal haitakua nje ya top 7 lakini hata kama itakuepo unadhani gape la kutoka walio juu yake mpaka yeye litakua lipoje? City katumia almost 1B United katumia almost 1B.
Arsenal atakua katumia sh ngapi? Madirisha ya usajili mangapi arsenal alitangaza kua na 200M za usajili? City anasajili beki wa 60M anagundua ni kinabo, anasajili wa 40M anagundua ni kinabo anasajili wa 20M ndiyo anakua stopa ile 100M inaachwa ipashe joto benchi.
Ni kama darasani niwe wa pili katika matokeo ila nina 30 wakati wa kwanza ana 80, haimake sense. Kua wa pili won't matter kwa gape kama hilo.