Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Hii team inachosha yaani hiki kitambi changu nilicho kipata ndani ya miezi mitatu hii, kitapotea ndani ya wiki moja, hapo bado Chelsea na City daaaaah.......

Hivi huyu Kroenke anatutakia nini si aondoke manake anang'ang'ania timu na hataki kuweka hela,yaani kama ikiwezekana wamloge atuachie timu yetu.

Tutamlaumu Arteta sawa lkn hata akija kocha mpya still hatopewa fungu la kutosha la usajili.Yaani mashabiki wa Arsenal kwa sasa tulivyo ni kama wale wasabato masalia waliotaka kusafiri ulaya bila passport wala nauli,tusijipe imani timu hatuna, kocha hatuna na Kroenke mbahili.
Nilikuwa naandika kwa kuwabeza humu, Ila hii comment imenigusa Sana! Tatizo wengine wenzako wanajifariji kwamba Mambo yako shwari, ilihali sio hivyo!

Pole Sana mkuu!
 
Hii team inachosha yaani hiki kitambi changu nilicho kipata ndani ya miezi mitatu hii, kitapotea ndani ya wiki moja, hapo bado Chelsea na City daaaaah.......

Hivi huyu Kroenke anatutakia nini si aondoke manake anang'ang'ania timu na hataki kuweka hela,yaani kama ikiwezekana wamloge atuachie timu yetu.

Tutamlaumu Arteta sawa lkn hata akija kocha mpya still hatopewa fungu la kutosha la usajili.Yaani mashabiki wa Arsenal kwa sasa tulivyo ni kama wale wasabato masalia waliotaka kusafiri ulaya bila passport wala nauli,tusijipe imani timu hatuna, kocha hatuna na Kroenke mbahili.
Niuzien mm hii timu hamtaki?

Ngoja nijaribu Tena mwaka huu kuinunua

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kwa kunidai ushahidi usio na shaka utakuwa ama umedhamiria kunizuia kujadili au umeamua 'kunikomesha' tu, ha haaaa!!

On a serious note, taarifa zilizoripotiwa na media zenye kuaminika kwa habari za michezo ikiwemo goalnews.com ziliripoti kuwa Luis Enrique alihitaji £250m za usajili huku akieleza kuwa ni wachezaji sita tu wenye uhakika wa kupata namba kikosi cha kwanza na wengine watahitaji kuraise their standards to convince him.


Hii ni normal situation kwa vilabu vingi tu, kama hujaweza kumuuza mchezaji usiemtaka kikosini, kuliko kukaa naye umlipe full salary ni more economy kumtoa kwa mkopo then mnashare salary huku akipata game time kutunza/kukuza uwezo wake na thamani yake pia ili hata ukitaka kumuuza upate hela nzuri.


Hili pia ni kawaida anapokuja kocha mpya, wapo wataondoka, wapo watabaki na wapo wa bench wataaminiwa kutokana na philosophy ya kocha husika, by the way Saliba hakusajiliwa na Arteta.

Hili acha na me nikurudishie 'kibano' ulichonipa hapo juu, naamini huna ushahidi usio na shaka, ha haaaa!!

Kupigwa hela inaweza kutokea hasa kwenye situation tuliyopo (panic buy), lakini nayo imetokea watu wanalipa £50m+ for bench warmers. Katika hiki kipindi cha mawakala hilo linaweza kukukumba, sometimes mawakala wanawezesha deal kwa maslahi yao na sio vilabu.

Issue ya Martinez nadhani alipata nafasi kama mechi 7 hivi za mwisho baada ya Leno kuumia, unawezaje kumuamini kirahisi hivo kwa mechi 7? Huyu Martinez alikuwepo enzi za Wenger, Unai na hakuaminiwa kupewa namba. Infact Leno alinunuliwa kuwa namba 2 nyuma ya Cèch na yeye akiwemo, sasa mnatakaje Arteta amuamini kirahisi tu?


Tangu Kreonke achukue club hajawawi ku endorse pesa, hiyo unayoisema nyingi ni ambayo club imezalisha toka kwenye vyanzo vyake vingine.

Hizo pesa kweli ni nyingi lakini not well spent, unaweza kuwalaumu wanaonunua wachezaji lakini ukienda deep utagundua deals zetu nyingi hata cash hatuwezi kulipa tunalipa kwa installments, huo utaratibu wa malipo ambao timu nyingi haziutaki zimetufanya tushindwe kupata top target players ila tunanunua wale ambao wanakubaliana na taratibu zetu za manunuzi and that's down to the owner (Kroenke).
Screenshot_20210814-170334_Chrome.jpg
 
Mungu atunusuru tusishuke daraja baada ya mechi 3 tutakuwa na point 0 hilo halihitaji ubishi au kutokuwa na akili timamu ya kulitambua hilo!Maadui zetu wote wanafungua msimu na point 3 za Maana!na ndio wataunda Top 4 na Top 10.Weeekend njema
 
Kuna kocha tulihusishwa naye kabla ya Arteta ila sidhani kama hata alikua approached.

Hili la Saliba niliwahi lisema humu. Saliba na Fofana wametoka timu moja ambayo hiyo timu Saliba ni nahodha, kitakwimu Saliba kamuacha mbali Fofana na wa kwanza kuja EPL alikua Saliba.

Fofana amekuja ndani ya wiki mbili anagewa namba Leicester huku Arsenal wanasema Saliba hayupo tayari.

Kisha Saliba akarudi ligue 1. Mpaka ligi inaisha nafikiri hakuna aliyefanikiwa kumpita kwa kudribble.

Guendouz ana attitude nzuri. Shida yake ambayo kila siku naisema ni hana chochote kitakachomfanya awe starter day in day out, stamina hana, pace hana, skills hana, vision hana. Notice kwamba Emery kamtoa daraja la pili (au la tatu) Lokonga sijamuona akicheza ila stats zake zinaongea vizuri. Sidhani kama tumepotea kwa Lokonga.

White usajili wake ni wa kuziba pengo la Luiz ambaye kwa Arsenal alikua ndiye beki anayeweza piga long balls kuzidi waliokuwepo. Na White anaweza hizo long balls so usajili wake ni ule wa kutaka timu icheze kuanzia nyuma. (Maelezo siyo yangu)

50M is ridiculous but wote tunajua katika negotiation kuna vitu vinaangaliwa. Muda uliobaki katika mkataba, umri wa mchezaji na timu yake inamuonaje.

Odegaard kuanzia amekuja mpaka ameondoka ametengeneza nafasi nyingi kuzidi aliowakuta lakini kiukweli mi naona Odegaard ni mchezaji ambaye hakufanya nilichotarajia. Ama hivyo au kocha hajui jinsi ya kuextract potential ya mchezaji skilled kama yule.

So kwangu ni mchezaji ambaye ni bora aje tena ila kwa mkopo na option ya kununua iwepo ikatokea kuna vitu ametimiza.

Tuna Leno. Tumemaliza msimu timu ya tatu kufungwa magoli machache. Tuliowauzia Martinez wako wapi? Varane kwa pesa aliyouzwa imeonekana Madrid ni wajinga lakini wangekaza shingo angeondoka free kama Ramos na kama donnaruma. Na sisi yangetukuta. Martinez anahitaji kua starting XI ili apate namba Argentina.

Sidhani kama Arsenal haitakua nje ya top 7 lakini hata kama itakuepo unadhani gape la kutoka walio juu yake mpaka yeye litakua lipoje? City katumia almost 1B United katumia almost 1B.

Arsenal atakua katumia sh ngapi? Madirisha ya usajili mangapi arsenal alitangaza kua na 200M za usajili? City anasajili beki wa 60M anagundua ni kinabo, anasajili wa 40M anagundua ni kinabo anasajili wa 20M ndiyo anakua stopa ile 100M inaachwa ipashe joto benchi.

Ni kama darasani niwe wa pili katika matokeo ila nina 30 wakati wa kwanza ana 80, haimake sense. Kua wa pili won't matter kwa gape kama hilo.
Leno tatizo mkuu, anadisconnect timu na jana kajiExpose mno kila mtu kaona,

Kajaribu kuangalia Build up ya Emi Martinez youtube kipindi tunachukua FA afu ufananishe na Leno utaona GK ni shida kuliko.
 
Leno tatizo mkuu, anadisconnect timu na jana kajiExpose mno kila mtu kaona,

Kajaribu kuangalia Build up ya Emi Martinez youtube kipindi tunachukua FA afu ufananishe na Leno utaona GK ni shida kuliko.
Huyo mnayesema anajua kuliko Leno tayari katobolewa mara tatu na Villa ni miongoni mwa timu zilizofanya poa sokoni
 
Mungu atunusuru tusishuke daraja baada ya mechi 3 tutakuwa na point 0 hilo halihitaji ubishi au kutokuwa na akili timamu ya kulitambua hilo!Maadui zetu wote wanafungua msimu na point 3 za Maana!na ndio wataunda Top 4 na Top 10.Weeekend njema
Dah, umeongea kwa uchungu sana mkuu. Pole sana yaani
 
Back
Top Bottom