Ukiwa na striker mzuri unaweza kujiamini na mid ya sasa.
Watu wengi hatukua tunajua ila mechi za pre season zimetuonyesha Sambi Lokonga ni mchezaji wa aina gani.
Lokonga ni Vieira na Fabregas ndani ya mtu mmoja anakukaba usipite lakini hashindwi kupangua watu na kutoa pasi ya goli au hata yeye mwenyewe kufunga.
Yaani ni kwamba pale katikati akiwepo Partey na Lokonga kinachohitajika ni mtu wa mbele kua fasta. Martinell ni jibu, Balogun ni jibu, Nketiah ni jibu mashindano ya FA na Carabao yataprove ninachosema.
Mpira wa siku hizi unawapa majukumu mawinger, Villa walimtaka Emile, wamemkosa wamemfuata Bailey. Baadhi ya timu zimewaconvert mawinga wao kua viungo washambuliaji mfano Villa kwa Grealish, Leicester kwa Maddison na Arsenal kwa Emile. Timu zingine zimewafanya mastriker kabisa mfano PSG kwa Mbappe, Inter na Lautaro, Madrid na Ronaldo.
Emile angeenda Villa angedevelope vizuri kwakua presha ndogo na style yake ya kufanya runs ni nzuri kwa Villa wanaocheza counter na penetration pass hapa presha ipo juu so anatakiwa awe nunda kabla ya wakati, na style yetu ya back passes na sideway passes inamfanya aonekane ana mchango wastani hii inaweza kufanya mashabiki tusiwe na shukrani na juhudi atakazoonyesha.
Kama Lokonga atakua na kiwango nusu na robo ya tulichoona kitakwimu hicho hicho kitamtosha Emile. Tavarez is gud, no worries kule kushoto. Pepe ameminya purple patch tumemaliza msimu ameanza kua moto.
So nafikiri kiukweli ukweli anahitajika ST. Atafutwe Luca Jovic aje pale kwa mkopo.