Usajili Update....
Arsenal bado inaendeleza mazungumzo ya mkataba mpya na Emile Smith Rowe. Fabrizio Romano anasema pande zote mbili zinahitajiana na Emile anataka kubaki Arsenal hivyo ni swala la muda tu.
Bissouma anahitajika na Arsenal ila siyo kipaumbele kwa eneo hilo kwa kua Arsenal ina wachezaji inaowapigia hesabu.
Arsenal walipeleka ofa Sheffield kwa ajili ya Sander Berge lakini Sheffield wanataka ofa ya kuanzia paundi Milioni 30.
Ceballos kuondoka Arsenal ni uhakika kwa 100% ameamua arudi Madrid ili akagombee namba ikitarajiwa Modric na Kroos wataondoka Madrid.
Kuna tetesi zenye nguvu zikisema Bellerin anaenda PSG. Ila hata kama siyo PSG ni inadhaniwa anaondoka.
Atletico bado wanamfukuzia Lacazette.
David Luiz amethibitisha kuondoka na amewaaga mashabiki kupitia mtandao wa Twitter. Sead Kolasinac anatarajiwa kurudi Arsenal baada ya mkopo wake kuisha Schalke, timu mbili Schalke na Lazio wote wameonyesha kumtaka hata hivyo Schalke wapo tayari kutoa paundi milioni 1 na nusu tu.
Arteta amesema Willock anarudi Arsenal. Ramsey amesema anataka kurudi Arsenal ila Arsenal hawajasema chochote.
Aouar amesema anataka kuhama timu na inatarajiwa Arsenal kupeleka ofa yao.
Hata hivyo Kroenke aliyeahidi kutumia pesa nyingi kusajili ameshindwa kulipa deni la paundi milioni 120 la msaada wakati wa corona na badala yake ameenda kukopa benki ili kulipa hilo deni. Hivyo bado Arsenal ina deni, wakati anafanya hivyo ametumia pesa nyingi kujenga uwanja kwa timu yake nyingine iliyo Marekani, kwa ajili ya hiyo timu ametumia zaidi ya dola Bilioni (Siyo Milioni) 1.
Kroenke out.
Tusubiri fununu zingine.