Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Bora kucheza futuhi kuliko hili kombe la viti maalum humu watakutana na wakina lens, Riga, Suduva, Aberdeen, Shamrock Rovers, Sarajevo, levsci Sofia hatari saaaaana
Mashindano ya kubeti hayo
 
Timu yenye jina huwezi kulitamka unabet imefungwa
Hivyo vitimu vidogo ndio vina matokeo ya uhakika. Mi siku nikiwakuta rigas futibola skola (RFS), Dudelange, fola, B36 Torshavn, Runavik, KR Reykjavik, gyirmot, Debreceni, slovan Bratislava... Hapo naweka 2.5 over wote
 
Hahaha hapo nimeona ni timu mbili tu nimewahi zishuhudia zikicheza. Bratislava na Dudelange tena ilikua marudio
 
Kaka umerudi? Karibu sana
Yap, pamoja sana.
Lakini naona munamaliza ligi katika nafasi za kinyonge.
Hii inadhihirisha ile safari yenu ya kuifuata Sandalend ilipo ime pamba moto.
 
Yap, pamoja sana.
Lakini naona munamaliza ligi katika nafasi za kinyonge.
Hii inadhihirisha ile safari yenu ya kuifuata Sandalend ilipo ime pamba moto.
We kaka, sio huku bhana, mbona unapiga kwenye mshono?
 
Yap, pamoja sana.
Lakini naona munamaliza ligi katika nafasi za kinyonge.
Hii inadhihirisha ile safari yenu ya kuifuata Sandalend ilipo ime pamba moto.
We chapati sisi tulishasema lengo la timu yetu miaka miwili ya kwanza ni kipigo kwa chelsea na united tu yale makombe tulibeba bahati mbaya.

Mwakani ndiyo tunaanza kutafuta makombe. Kipaumbele kitakua siyo kipigo kwa united na chelsea
 
Duh! Mrembo kama ww unabet.!?
Hivyo vitimu vidogo ndio vina matokeo ya uhakika. Mi siku nikiwakuta rigas futibola skola (RFS), Dudelange, fola, B36 Torshavn, Runavik, KR Reykjavik, gyirmot, Debreceni, slovan Bratislava... Hapo naweka 2.5 over wote
 
Washika bunduki hamjambo?
20210506_235439.jpg
 
Leo inatakiwa tushinde. Bila kujali matokeo ya wenzetu ni tunatakiwa tushinde.
 
Arsenal, Chelsea and Tottenham are reportedly all set for talks with the Premier League next week to find out their punishment over the controversial European Super League plans.
According to Sky Sports, the Premier League will hold talks with the Gunners, the Blues, Spurs, Manchester City, Manchester United and Liverpool next week over fines that could total to tens of millions of pounds.
It has also been claimed that the top-flight are considering a one-off fine, or perhaps a smaller payment from the clubs, as well as a share of next season's broadcast income.

An initial proposal made from the Premier League earlier this month had plans of a £15m fine per club, as well as a suspended points deduction, the article states
 
Uko vizuri pande za uwekezaji
Hivyo vitimu vidogo ndio vina matokeo ya uhakika. Mi siku nikiwakuta rigas futibola skola (RFS), Dudelange, fola, B36 Torshavn, Runavik, KR Reykjavik, gyirmot, Debreceni, slovan Bratislava... Hapo naweka 2.5 over wote
 
Usajili Update....

Arsenal bado inaendeleza mazungumzo ya mkataba mpya na Emile Smith Rowe. Fabrizio Romano anasema pande zote mbili zinahitajiana na Emile anataka kubaki Arsenal hivyo ni swala la muda tu.

Bissouma anahitajika na Arsenal ila siyo kipaumbele kwa eneo hilo kwa kua Arsenal ina wachezaji inaowapigia hesabu.

Arsenal walipeleka ofa Sheffield kwa ajili ya Sander Berge lakini Sheffield wanataka ofa ya kuanzia paundi Milioni 30.

Ceballos kuondoka Arsenal ni uhakika kwa 100% ameamua arudi Madrid ili akagombee namba ikitarajiwa Modric na Kroos wataondoka Madrid.

Kuna tetesi zenye nguvu zikisema Bellerin anaenda PSG. Ila hata kama siyo PSG ni inadhaniwa anaondoka.

Atletico bado wanamfukuzia Lacazette.

David Luiz amethibitisha kuondoka na amewaaga mashabiki kupitia mtandao wa Twitter. Sead Kolasinac anatarajiwa kurudi Arsenal baada ya mkopo wake kuisha Schalke, timu mbili Schalke na Lazio wote wameonyesha kumtaka hata hivyo Schalke wapo tayari kutoa paundi milioni 1 na nusu tu.

Arteta amesema Willock anarudi Arsenal. Ramsey amesema anataka kurudi Arsenal ila Arsenal hawajasema chochote.

Aouar amesema anataka kuhama timu na inatarajiwa Arsenal kupeleka ofa yao.

Hata hivyo Kroenke aliyeahidi kutumia pesa nyingi kusajili ameshindwa kulipa deni la paundi milioni 120 la msaada wakati wa corona na badala yake ameenda kukopa benki ili kulipa hilo deni. Hivyo bado Arsenal ina deni, wakati anafanya hivyo ametumia pesa nyingi kujenga uwanja kwa timu yake nyingine iliyo Marekani, kwa ajili ya hiyo timu ametumia zaidi ya dola Bilioni (Siyo Milioni) 1.

Kroenke out.

Tusubiri fununu zingine.
 
Back
Top Bottom