Jana Leicester kashinda.
Kwa aliyetoka kumfunga Leicester hakuna aliyedhani angeshinda kwa United. Kabla ya game Ole alinukuliwa akisema kwa hizi mechi zinazoikabili United itabidi afanye rotation ya mpaka anapokutana na Villar fainali.
Lakini katika ligi ya Uingereza ukiiondoa City ni Chelsea pekee ambayo inaweza kutoa mtu na kuingiza mtu mwenye uwezo unaokaribiana na anayetoka. Chelsea wana kikosi kipana, pengine ndiyo maana hatujamsikia Thomas akiongelea swala la kikosi.
Arsenal tunaingia kwenye hii game tukiwa underdogs na morali iko chini, msimu kwetu hauna maana tena, mara ya mwisho tulikutana naye tukiwa hatuna morali tumefululiza kufungwa, tukaifunga Chelsea 3 - 1.
Kipindi hiki kuigeuza mechi ni ngumu kiasi chake ila kwakua hatuna cha kupoteza iingie tu timu yenye akili ya kushambulia hamna kujibana bana Martinell na Pepe wenye akili ya kushuti hata nje ya box wawekwe, Auba anayeweza kucut in na kuscore awekwe.
Tuna majeruhi, Emile, Mari na Luiz ingawa Emile na Mari wanaweza kuanza, Luiz ni uhakika kwamba hayupo.
Saa 4 siyo mbali.