Matchday vs Everton.
Hii ni second leg. First leg Everton alitupiga 2 kwa 1. Katika hiyo game kila mmoja angeweza kushinda ila Everton aliondoka na ushindi.
Leo tunaingia huku tukiwa na majeruhi Alex, Pierre, Martin, Kieran na David. Wengine hapo ni hawawezi kucheza wakati baadhi wanaangaliwa kama wataweza kuwepo kikosini.
Carlo ni kocha mzuri, ameprove mara nyingi uzoefu wake ni silaha, kafanya hivyo kwa Liva na kafanya hivyo kwa United kisha akafanya hivyo kwetu so ni game tight kimtindo ukizingatia kocha ana kazi ya kuwalinda wachezaji wetu kwaajili ya Alhamisi.
First XI nafikiri itakua vyema beki ikimjumuisha Cedric ili mashambulizi yaanzie nyuma na awepo beki anayeweza kuoverlap ili kutanua uwanja. Game iliyopita Elneny hakua mwiba sana nadhani leo anaweza asianze hivyo awepo Dani na Partey katikati au Granit na Partey.
Forward iwe na Pepe, Saka, Emile na Martinell.
Tukutane saa nne.