Man United kuwa wa kwanza ni kama kumuona tembo juu ya mti. Wote hatujui kapandaje ila tuna uhakika atashuka.
Kwa kuzingatia game yao na Liva, kikosi chao na majeruhi yetu niliona tuna asilimia 30 kushinda. 30 kusuluhu na wao wana 40 za kushinda.
Ila kwa game yao ya jana hapana. Morali yao itakua imesheki vibaya.
Arsenal tunaenda na ushindi wetu kwa Soton tulioupata kwa comeback, tena huu ushindi Emile hakutoa assisst that means kwa sasa tushajijua kua ukipata mpira pasi ni mbele.
Kuna Odegaard, Pepe kapafom vizuri, Saka is on fire hawa wote wanaweza kucheza RW ila Saka kajimilikisha hiyo namba kwa sasa. So Arteta anaweza kumuweka tena Pepe LW, Saka RW na Odegaard AM.
Ingawa kama Emile anaweza kucheza nitaona ni sawa zaidi akianza as kumuamini mgeni straight away kwa game kama hii kunashusha morali ya mwingine.
Nafikiri hii game Gabriel ataanza.
Kuna game moja Partey na Elneny walitawala dimba la kati hadi nikaona wivu sijui kwanini hii duo haijawahi kurudia kile kiwango.
Soares is good, in fact Tierney akirudi ni sawa Soares akibaki kulia tushuhudie atakacholeta uwanjani.
Hii game tuna uwezo wa kushinda.