Arsenal (The Gunners) | Special Thread

George Ambangile
Southampton walikuwa dhofu , katika maeneo yote wakiwa na mpira na hata bila mpira . Na Arsenal hawakuhitaji hata kubadilisha gia kuwafumua Soton leo . Walichofanya vijana wa Arteta ni kufanya mambo ya msingi kwa usahihi ( Do the basics right ) : Pasi sahihi, mikimbio sahihi, pressing kwa wakati sahihi na kuilinda shepu ya timu vizuri ( keep the shape ) .
Ukiacha goli alilofunga na assist yake kwa Saka, nimependa sana jinsi Alex Lacazette alivyokuwa anafanya “ Shadow Pressing “ dhidi ya Ward Prowse : kwamba alikuwa anaruhusu mabeki wawe na mpira lakini alikuwa anafunga njia ya pasi kwenda kwa Ward Prowse ambaye alikuwa nyuma yake . Maana yake mabeki wa Soton walilazimika kupiga pasi kwa mabeki wa pembeni na hapo ndio Saka , ESR na Pepe walipokuwa wanavamia kwa nguvu kuiba mipira . Magoli 8 ya EPL mpaka sasa kwa Lacanyavu.
Kama unacheza na washambuliaji wawili mbele ( Adams na Ings ) halafu mipira kutoka kwa mabeki wako kwenda kwa viungo inawachelewa maana yake kazi ya Holding na Luiz inakuwa nyepesi sana . Laca , Xhaka na Partey waliharibu mpango huo wa Soton na ilikuwa rahisi hasa ukizingatia viungo wa Sotob hata wakipata mipira , pasi ni MKAA .!
😀

NOTE:
1: Nitashangaa sana kama Bukayo Saka mwisho wa msimu asipotwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa mwaka . Kila siku performance zake utasema mchezaji mzoefu wa miaka 28 .
2: Cedric Soares kuna baadhi ya pasi alikuwa anapiga ni kama kiungo wa kati kwenda kwa Saka . Na pia alimuweka Walcott kwenye mfuko mdogo wa Jeans .
3: Labda ni Amstrong pekee ndio anaweza kutoka uwanjani kichwa juu katika kikosi cha Soton .
Full Time : Soton 1-3 Arsenal

Kwenye uzi wenu niliwahi kuandika hivi

United kua wa kwanza ni kama kumuona tembo juu ya mti. Wote hatujui kapandaje ila tuna uhakika atashuka.

Now to be fair mnaongozwa na bahati kipindi hichi, mnafuatwa na game nyanya baada ya Arsenal hamna majeruhi so mko tayari kushika tena nafasi ya kwanza au siyo?

Hehehe, sheffield ikitoka kwenu inaenda kwa City, leo leicester akishinda united inashuka mpaka nafasi ya tatu. Kisha ili iwe ya kwanza itabidi imfunge Arsenal.

Kazi au?
partey hajaumia sana, emile pia, ila tyra odegaard kaja muda muafaka...

auba anapitia hali ngumu kifamilia, nimependa jana wachezaji karibu wote wameonesha love kwa auba, jamaa huwa ni mtu wa furaha muda wote... sasa sijui amekumbwa na nini dah...
 
Top 4 ni ngumu. Angalia games tano zinazofuata

Arsenal V man united.

Wolves V Arsenal

Aston Villa V Arsenal

Arsenal V Leeds

Arsenal V City

Katika hawa 5 tumemfunga united na kusuluhu na leeds waliobaki walitupiga. Na hizi ndiyo games ambazo tukishinda tunajikuta ndani ya top 4.

Tatizo tulilonalo kipindi hichi ni majeruhi yasiyoisha, unamuona Mari wiki mbili kisha unasikia kajeruhiwa. Unamuona Tierney naye same shit.

Partey na Emile jana wameumizwa pia. Hapo bado hatujui Tierney anarudi lini, nilisema hawa 3 pamoja na Saka na Laca ndiyo chachu ya ushindi sasa wanabaki watu 2 kama chachu ya ushindi its weird.

Arsenal imesajili physio mpya pengine kukabiliana na hili swala ila obviously haisaidii. Ninachohofia ni kujikuta tunarudi 3 4 3 ili kuziba pengo la LB.

Pia notice kwamba kati kati ya hiyo wiki ya hizo games tano tuna game na Benfica ya home and away, now tunawezaje kugawa hichi kikosi kiperform katika tournaments zote? Na hapo ni bora hatupo FA wala EFL la sivyo mtihani ungekua mkubwa zaidi.

Baada ya hizi games 5 wanakuja wakina Leicester kisha tutaanza kukutana na chai za maziwa. Ila ni mpaka mwezi wa nne. So kama unataka kuyeyuka kwenye huu uzi yeyuka tu utaibuka mwezi wa tano ukiwa sure na ushindi.
Kt jana angeweza kucheza ila naona kama walichukua tahadhari kuelekea trh 30, emile, na partey....partey ni just clamp, emile ndio kuna wasiwasi kidogo... but odegaard kaja muda muafaka

hizi game 5 ni za kulipa visasi hasa villa na wolves ..... leicester hadi leo sielewi alitufungaje japo tatizo kuu lilikuwa AM
 
Walipaki basi.

Mid ya kusakama lango haikuepo, ikapigwa kaunta Mustafi akashindwa kudefend Vardy akamaliza. Tena ilikua dakika za 87 kuendelea.
 
United kuWa wa kwanza ni kama kumuona tembo juu ya mti. Wote hatujui kapandaje ila tuna uhakika atashuka.

Castr
Hii timu morali ikisheki tu watajikuta pabaya, leo Sheffield sidhani kama atapona.

Ila unajua kuna watu kila wanachobeti hua kinaenda kinyume? Mfano Pele akisema timu fulani itachukua kombe ujue inatoka hatua za mtoano tu atakayoitabiria mabaya hufika mbali.

Kama unamjua mtu yeyote mwenye hii sifa, mwambie abet united inashinda.
 
Walipaki basi.

Mid ya kusakama lango haikuepo, ikapigwa kaunta Mustafi akashindwa kudefend Vardy akamaliza. Tena ilikua dakika za 87 kuendelea.
naona Arteta hataki kabisa kumsikia mustafi, ...naomba partey awepo, pengo la emile tunaweza kumpa odegaard.... mari awe amerudi, wacheze na holding...luiz haaminiki
 
Arteta kuhusu Odegaard:

"Nafikiri tunakaribia kumsajili lakini bado hatujakamilisha kwa ninavyo elewa. Sijaongea na Edu wala mtu yoyote klabuni ndani ya saa chache za mwisho lakini tuna uhakika kwamba tutakamilisha dili"
 
Top 4 ni ngumu. Angalia games tano zinazofuata

Arsenal V man united.

Wolves V Arsenal

Aston Villa V Arsenal

Arsenal V Leeds

Arsenal V City

Katika hawa 5 tumemfunga united na kusuluhu na leeds waliobaki walitupiga. Na hizi ndiyo games ambazo tukishinda tunajikuta ndani ya top 4.

Tatizo tulilonalo kipindi hichi ni majeruhi yasiyoisha, unamuona Mari wiki mbili kisha unasikia kajeruhiwa. Unamuona Tierney naye same shit.

Partey na Emile jana wameumizwa pia. Hapo bado hatujui Tierney anarudi lini, nilisema hawa 3 pamoja na Saka na Laca ndiyo chachu ya ushindi sasa wanabaki watu 2 kama chachu ya ushindi its weird.

Arsenal imesajili physio mpya pengine kukabiliana na hili swala ila obviously haisaidii. Ninachohofia ni kujikuta tunarudi 3 4 3 ili kuziba pengo la LB.

Pia notice kwamba kati kati ya hiyo wiki ya hizo games tano tuna game na Benfica ya home and away, now tunawezaje kugawa hichi kikosi kiperform katika tournaments zote? Na hapo ni bora hatupo FA wala EFL la sivyo mtihani ungekua mkubwa zaidi.

Baada ya hizi games 5 wanakuja wakina Leicester kisha tutaanza kukutana na chai za maziwa. Ila ni mpaka mwezi wa nne. So kama unataka kuyeyuka kwenye huu uzi yeyuka tu utaibuka mwezi wa tano ukiwa sure na ushindi.
Amini nakwambia Arsenal hii kweli ni dhaifu kiasi ila pia ni timu ambayo haitabiriki kabisa nani alitegemea jana Southampton watatoa ulimi nje tena kwao?
Amini nakwambia hapo mechi ngumu ni dhidi ya Manchester City peke yake trust me and Mark my words
 
Alexandre Lacazette and Bukayo Saka both sent messages of support to Pierre-Emerick Aubameyang after their goals against Southampton.
Mikel Arteta: “I love how they support each other and protect each other.
"Auba is having a difficult time, we're all behind him and this win is for him."

Auba amekutwa na msala gani ?
 
Amini nakwambia Arsenal hii kweli ni dhaifu kiasi ila pia ni timu ambayo haitabiriki kabisa nani alitegemea jana Southampton watatoa ulimi nje tena kwao?
Amini nakwambia hapo mechi ngumu ni dhidi ya Manchester City peke yake trust me and Mark my words
Umeconsider majeruhi?
 
Back
Top Bottom