Kesho tunaanza kampeni ya kutetea kombe la FA. Tumetoka kushinda games tatu mfululizo baada ya Emile kuanzishwa, so imani ya wengi ni uwepo wake ni mchango kwa ushindi wetu.
Kibaya zaidi tunakutana na New Castle ambaye ni mwanaligi mwenzetu so unaona jinsi gani Emile anahitajika hapa. Ila baada ya hii game inafuata game ya ligi na Palace, mashabiki na timu kwa ujumla inahitaji zaidi ushindi kwenye ligi. Hivyo kumchosha au kumrisk Emile haitakiwi.
Lakini kwa userious wote. Tunashinda kwakua Emile ni mzuri kiasi hicho? Mi naona hana uzuri kiasi hicho ila hasiti kusprint na kusogea mbele. Katika games tulizoshinda tulikua na winning probability kubwa kuliko wapinzanji, sababu pekee hatukua tunashinda ni wachezaji kutokua na hamu ya kusogea mbele.
Swala linaloonekana wazi goli la pili dhidi ya West Bromwich.
So Emile apumzike, atahitajika siku ya Palace ila kwa kesho atafutwe mwenye maono na hamu ya kwenda mbele mwingine.