Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mkuu na we unakua mgeni ktk soka nn? Starting lineup itatokaje sahv ilihali game inachezwa SAA 2:30 huko?
Pengine labda nimekosea kuuliza swali, ilitakiwa niuulize possible starting line up

Na sio lazima itoke muda mchache kabla ya game, mbona ni kawaida sana kutoa hasubui na game inapigwa jioni
 
Kwahiyo mzee baba umehama kabisa Zebra United au ni kwa kipindi hiki tu
Kufukuza kocha siyo issue. Issue ni picha kubwa inayoambatana na kubadili kocha. Timu inapobadili kocha inabidi ijue pia itapaswa kuingia kwenye mradi mpya wa usajili. Mfano mzuri ni Liverpool. Walipoamua kuingia kwenye project mpya (2015) walitafuta kocha anayeendana na wanachotaka. Wakaanza kumpa kikosi anachotaka taratibu.

Imewachukua Liverpool misimu minne kuanza kuvuna walichopanda. Klopp hakuanza kupata mafanikio mpaka pale alipopata mchezaji wa mwisho aliyemtaka (kipa). Ungedhani kuwa Liverpool iko tayari kushindana baada ya kumsajili VVD, lakini bado kipa aliwaangusha. Walianza kutwaa mataji baada ya kuleta kipa ghali zaidi duniani wakati wakimsajili.

Angalia Spurs (japo wengi mnawadharau ila project yao ni master class). Baada ya kukamilisha project ya uwanja na kwamba project yao ya awali na Poch (ya wachezaji 7; akina Son, Dele, Kane, Lamela, Dier, nk) ilikwisha anza kuzeeka wakaamua kuingia kwenye project mpya ya kujenga kikosi.

Lakini walijiuliza ikiwa Poch ndiye kocha sahihi kulingana na malengo yao. Wakaona wamfute kazi kocha aliyetoka kuwafikisha fainali ya uefa ambayo hakuna aliyetarajia! Wakaona wamwajiri Mourinho lakini wakijua fika atataka kikosi chake.

Levy alimbipu Jose kwenye dirisha la January kwa kumpa wachezaji wasio chaguo lake. Jose hakujibu akaacha wajijibu wenyewe (kati ya sajili tatu; Bergwijn, Gedson na Lo Celso, ni moja tu inayofanya kazi, ya Lo Celso).

Dirisha lililofuata wakampa wachezaji 7 wapya na sasa Spurs ndiyo timu inayoogopwa zaidi (kimatokeo: achana na habari za beautiful football). No dhahili pia kuwa January ijayo watampa anachotaka yaani beki ya kati inayocheza kuchoto.

Ukijumlisha sajili za mwaka mmoja wa kwanza wa Jose ni wachezaji 10!

Sasa swali kwenu Arsenal mnaotaka Arteta aondoshwe, je timu yenu ina ubavu na utayari wa kumpa kocha mpya kikosi anachotaka? Kama jibu ni hapana basi mjue atakuja kocha mpya, atapewa wachezaji wawili watatu ili mgt ijivue lawama kisha naye hamalizi misimu miwili.

Huo ugonjwa wa poor planning ndiyo pia unaitafuna timu yangu ya zamani. Na yenyewe tangu babu astaafu malengo yake ya msingi ni kukuza zaidi biashara kuliko soka huku wakifanikiwa kuwahadaa mashabiki kwa kujificha kwenye kichaka cha "beautiful attacking football".
 
Ndiyo hivyo tushamalizana jana na sasa wote tunaongea lugha moja. Mkubwa keshajulikana. Wewe pia tulikukosa nyumbani kwako sasa mechi ijayo usitarajie kukutana na ile defense dhaifu ya Eric Dier na yule dogo Rodon ambaye alicheza kwenye nafasi isiyo yake na bado akina Tammy wakashindwa kufunga.

Mechi ijayo tutakuwa na Milan Skriniar kushoto na Toby kulia. Hapo hakuna cha kaptein Amerika wala Kai nani atayetusumbua.
Nilifanya makosa sana siku ile kukuacha hivihivi na ndio unaanza kunitambia hapa☹️☹️

Shughuli yako inakuja lazima heshima irudi
 
Pengine labda nimekosea kuuliza swali, ilitakiwa niuulize possible starting line up

Na sio lazima itoke muda mchache kabla ya game, mbona ni kawaida sana kutoa hasubui na game inapigwa jioni
WE ulisikia wapi......Sijawahi kuona hyo kitu labda hapa bongo....kwamba game inachezwa jioni afu official starting eleven inatoka asubuhi....labda ligi za china
 
Kuna watu waliibuka kipindi fulani wakasema msimu huu kombe letu. Sijui wamepotea wapi.

Arsenal ni timu kubwa sana hii rough road inayopitiwa saa hii haitaiangusha Arsenal. Wataanguka makocha, bodi, wamiliki na wachezaji lakini hii timu itabaki hapa.

So kama kuna nigga anatarajia timu kuyeyuka kama Kajumulo FC miaka ya 2000 kwa Arsenal hapana, too much a giant kurudishwa chini. Timu kubwa hushuka daraja kwa sababu nyingine nyingine ila siyo kufungwa. Juve, Inter na wenzao hiko ndiyo kiliwatoa serie A na siyo vipigo.

Kuanzia 2008 mpaka 2014 liva ilikua inashika nafasi ya 6, 7 na 8 lakini wote tulijua haitashuka daraja. So hatutashuka daraja lakini ili kujinasua inabidi tupitie ruti wanazopita wenzetu.

Liva ilinunuliwa na wamiliki wapya cash ikamwagwa.

Chelsea ilinunuliwa na wamiliki wapya cash ikamwagwa.

New Castle hiyo ruti wamebaniwa.

Wolves ina wamiliki wapya ambao demand yao ni timu kubaki ligi kuu tu.

Levy kajiongeza kwa kumwaga cash.

Everton, Aston n.k

Van Gaal alisema kwa United ilikua ngumu kutoboa kimpira as CEO wao hana historia na mpira hata wetu ni hivyo pia hajali kitu kuhusu mpira.

Tunahitaji mwingine mwenye maono zaidi anayejua what matters in football.

Morali ya timu is shaken.
 
Adjustments.jpg
 
Ukiwa unacheza PES au FIFA iwe ya PS 4 au 3 halafu unatamani utumie kikosi chetu katika hiyo game tumia 4 3 1 2.

LB anakua Tierney.

CB ni Gabriel na Luiz.

RB Bellerin.

CDM Elneny

CM Partey na Ceballos.

AM Pepe

ST Auba na Laca.

Subs: Nketiah, Willian, Runarrsson,Nelson, Willock, Niles

Kwenye PES set

Attack : Tiki Taka.
Maintain formation.
Support level 50%

Defense: Deep Defensive Line.
Defense line unaishusha mpaka bar mbili.

Kwenye FIFA
Defense: Balanced
Attack: Balanced.

Anza kugawa vipigo.
 
Kwahiyo mzee baba umehama kabisa Zebra United au ni kwa kipindi hiki tu
Ha ha haa. Mie ninayo falsafa yangu moja hiyo. "Huwa sikai upande mmoja na kitu ambacho hakitafuti mafanikio". United ilinitesa sana kwani hata Woodward kaendelea kusisitiza hapo juzi kati kuwa malengo yanatekelezwa vizuri kabisa; kujenga timu kupitia vijana chipukizi, kucheza mpira wa kushambulia, na kucheza mpira unaovutia!

Sasa mimi nilizoea kipindi cha SAF lengo lilikuwa ni moja tu, kushinda mataji. Iwe kwa kushambulia, comeback, au kilinda goli moja kama mwali vile. Kwa hiyo baada ya kuvumilia vituko vya timu kwa miaka 6 tangu 2013 mpaka 2018 nikasema inatosha mimi nimezoea kushangilia timu inayolenga mafanikio ya uwanjani.

Bahati nzuri nikaishia kuipenda project ya Spurs. Siyo shabiki maandazi! Ni Spurs asilimia .

Kwa kifupi ni hivyo. Nipo sana tu.
 
Nilifanya makosa sana siku ile kukuacha hivihivi na ndio unaanza kunitambia hapa

Shughuli yako inakuja lazima heshima irudi
Msimu uliopita mlibahatisha kwa kuwa timu ilikuwa ya kuungaunga ila msimu huu, ngoja kwanza nicheki game na nyie lini niandae mahindi ya kukaanga mapema. Moja baada ya jingine, mjini wanayaita pop kon.
 
Mbona kwenye picha yenu hamna kombe? Wekeni hata chupa za chai
We bwana wewe . Makombe yako mengi tu pale juu mwanzoni mwa "sredi" yetu sema ni makombe ya mbuzi kwa kweli. Sema siyo ishu maana hata Chelsea Jose alipoishika ilikuwa na kakombe kamoja tu tena ka miaka 50 iliyopita (nusu karne!).

Respect Jose
 
Kuna watu waliibuka kipindi fulani wakasema msimu huu kombe letu. Sijui wamepotea wapi.

Arsenal ni timu kubwa sana hii rough road inayopitiwa saa hii haitaiangusha Arsenal. Wataanguka makocha, bodi, wamiliki na wachezaji lakini hii timu itabaki hapa.

So kama kuna nigga anatarajia timu kuyeyuka kama Kajumulo FC miaka ya 2000 kwa Arsenal hapana, too much a giant kurudishwa chini. Timu kubwa hushuka daraja kwa sababu nyingine nyingine ila siyo kufungwa. Juve, Inter na wenzao hiko ndiyo kiliwatoa serie A na siyo vipigo.

Kuanzia 2008 mpaka 2014 liva ilikua inashika nafasi ya 6, 7 na 8 lakini wote tulijua haitashuka daraja. So hatutashuka daraja lakini ili kujinasua inabidi tupitie ruti wanazopita wenzetu.

Liva ilinunuliwa na wamiliki wapya cash ikamwagwa.

Chelsea ilinunuliwa na wamiliki wapya cash ikamwagwa.

New Castle hiyo ruti wamebaniwa.

Wolves ina wamiliki wapya ambao demand yao ni timu kubaki ligi kuu tu.

Levy kajiongeza kwa kumwaga cash.

Everton, Aston n.k

Van Gaal alisema kwa United ilikua ngumu kutoboa kimpira as CEO wao hana historia na mpira hata wetu ni hivyo pia hajali kitu kuhusu mpira.

Tunahitaji mwingine mwenye maono zaidi anayejua what matters in football.

Morali ya timu is shaken.
Kusoma koment kutoka kwa shabiki anayejua mpira kuna raha ya bwana. Ukweli mtupu. Hapo kwa Levy ongezea nyama kidogo. Jamaa ni football genius na malengo yake ni vyote viwili: Kufanikiwa uwanjani na nje ya uwanja. Hivyo kafanya ubahili kwa miaka takriban 10 ili kujenga miundombinu ya klabu (hasa uwanja) kisha sasa karudi kiwanjani.
 
Msimu uliopita mlibahatisha kwa kuwa timu ilikuwa ya kuungaunga ila msimu huu, ngoja kwanza nicheki game na nyie lini niandae mahindi ya kukaanga mapema. Moja baada ya jingine, mjini wanayaita pop kon.
Mimi ni shabiki wa damu siwezi hama timu yangu kwa matokeo mabaya ina maana wale mashabiki maandazi wa karne hii ya 21 wanaweza kuhama huwezi kumbadili chui ngozi yake au huwezi kubadili kabila lako au huwezi kumbadili mtoto wako wa kumzaa hii yote ni mifano ninakupa hili chama langu nimetoka nalo mbali sana toka 94 mpaka sasa na mpaka naingia kaburini nitabaki kuwa The Gunners au washika mtutu wa London mlio kuwa mashabiki maandazi mtaondoka na mtatuachia chama letu tutaendelea kusonga mbele hakuna barabara isiyokuwa na mabonde na milima ya kupanda na kushuka ninashangaa sana mwanaume mwenye mke na watoto analilia lia na kuhama timu eti kisa kufungwa hakuna timu isiyofungwa duniani kama wewe ni shabiki kindakindaki mwanaume lazima ukubali kuwa matokeo yapo aina tatu kushinda, sare na kufungwa haya yote ni matokeo lazima uyakubali.
Always I support The Gunners and London is Red for ever and ever!!
 
Back
Top Bottom