Sidhani kama Auba kawa butu ila ukiangalia stats zetu utaona tunatengeneza nafasi chache sana na mfungaji tunaye mtegemea ni Auba pekee hivyo hata wapinzani haiwapi tabu kumkaba mtu mmoja. Bado timu yetu haina good balance kati ya midfield na attacking.
Enzi za Wenger tushakua na strikers za kawaida sana ambazo ziliweza kufunga magoli mengi si kwa sababu walikuwa strikers wazuri, bali timu ilikuwa inatengeneza nafasi nyingi sn. Yaani mtu ana goli 15 ila kakosa clear chances kama 40 hivi.
Adebayor, Bendtner, Giroud hawa wote walikuwa wa kawaida sana ila waliweza kufunga kutokana na multiple chances. Wangecheza kipindi hiki, wangezidiwa magoli hata na makipa wa timu zingine.
Enzi za Wenger tushacheza na strikers kama Yaya Sanogo, Joel Campbell, Jeremy Alladiere na Chamack na bado tulikuwa tunashinda kutokana na chances nyingi tulozokuwa tukitengeneza