Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

lakini wamecheza vizuri sana mechi ya leo, timu ina uwiano mzuri sana kuanzia eneo la ulinzi hadi kiungo

Big matches Arsenal anajitahidi sana kucheza, nadhani kocha wao ni mzuri kwenye tactical games, shida ni kwamba hawana wachezaji, na kwa mfumo wa Arsenal wa ubahili wataendelea hivi hivi mpaka morale itaisha.
 
Nikuulize wewe?Saka unasema aanzie benchi?
bado hajawa mchezaji anayepaswa kubebeshwa majukumu mazito ya timu ndio maana nikasema hapo mwanzoni ni mchezaji anayepaswa atokee benchi.

unatafutaje ubingwa wa ligi kwa safu ya ushambuliaji inayomjumuisha saka kama ni mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza
 
Hili jukwaa ukipita katikati ya wiki utasema hakuna team inayoweza kuifunga arsenal maana upangaji wa kikosi na mauchambuz ya hapa na pale utakubali ila ukija siku ya mechi kila mtu analalamika kuliko mwenzake
Hahahaha. Ndiyo raha ya jukwaa boss. Ushabiki ndiyo huo sasa 😀😀
 
Ukiwakuta wanakuchambulia hiyo kiungo yao yaan huyo ceballos unaweza sema labda ni boonge la mchezaj kumbe waongowaongo tu mara hapa akae xhaka pale muweke El neny yaan full vurugu tu

Nataka na huyo patei sijui part aanze kucheza tujue kama wamepigwa kama walivyopigwa kwa komred kipepe
Unaongea kinafki mkuu, kama ni wa kiume chunga sana utajashikishwa
 
bado hajawa mchezaji anayepaswa kubebeshwa majukumu mazito ya timu ndio maana nikasema hapo mwanzoni ni mchezaji anayepaswa atokee benchi.

unatafutaje ubingwa wa ligi kwa safu ya ushambuliaji inayomjumuisha saka kama ni mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza
True ila kwa sasa utampata nani ?Auba Laca Pepe wote hao ni wachezaji wenye viwango vya Dunia sijajua tatizo lao ni nini kushindwa kuperform
 
ManUtd watufanyie mpango waliofanyiwa na Liverpool wasituache tuchekwe peke yetu 😀
 
bado hajawa mchezaji anayepaswa kubebeshwa majukumu mazito ya timu ndio maana nikasema hapo mwanzoni ni mchezaji anayepaswa atokee benchi.

unatafutaje ubingwa wa ligi kwa safu ya ushambuliaji inayomjumuisha saka kama ni mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza
Saka aaminiwe mkuu,game zote alizocheza anafanya wonders,

Angalia game ya West ham kaiamua yeye,angalia game ya leicester Carabao na hata game ya leo ni nani amemzidi Saka kucheza mpira?

Imefikia hatua mpira ukiwa kwa Saka tunafeel comfortable kuliko hata ukiwa kwa senior players.
 
True ila kwa sasa utampata nani ?Auba Laca Pepe wote hao ni wachezaji wenye viwango vya Dunia sijajua tatizo lao ni nini kushindwa kuperform
ndio maana nikazungumzia ishu ya bajeti, ukiangalia sajili alizozifanya mikel arteta takribani zote zimelenga maeneo muhimu ambayo yalihitajika kufanyiwa overhaul ila ufinyu wa bajeti unakwamisha mipango yake ya kujenga timu bora kwa muda mfupi.

lacazette tokea ahamie arsenal ameshindwa kufikia ubora wake ule ulioshuhudiwa olympique lyon na huu ni msimu wake wa nne kama itakuwa nipo sahihi
pepe naye anaingia msimu wa pili akiwa bado anahangaika kurudisha ubora uliopelekea asajiliwe kwa thamani kubwa.
 
Kwa walioangalia mechi bila kuhemkwa nadhani watakuwa wameona kitu cha tofauti kabisa kwa arsenal hasa dk za mwisho za kipindi cha kwanza na kipindi chote cha pili.

Gem ya leo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Liverpool maana tumeona wachezaji wakijiamini na kucheza bila tension hivyo wakaweza kuzuia makosa mengi yasiyo ya lzm.

Km nilivyosema mapema kuwa mechi ya leo ni kipimo sahihi kabisa kwa arteta hasa baada ya ile mechi ya liver ambae ni giant wa ligi alafu anakutana tena na giant mwingine ndani ya muda mfupi na kila mtu ameona jinsi vijana walivyocheza kwa moyo na kwa kujituma huku wakiwa na passion ya ushindi kitu ambacho ni kizuri sana kwenye football.

Sasa tukija kuangalia ni wapi tumekwama issue ni kwamba tumekwama kwa kiungo mshambuliaji na bila arteta atalifanyia ili kutengeneza combination nzuri kati ya partey, xhaka na ceballos na nina imani gem ijayo ya away dhidi ya Man u tutaondoka na matokeo
 
Saka aaminiwe mkuu,game zote alizocheza anafanya wonders,

Angalia game ya West ham kaiamua yeye,angalia game ya leicester Carabao na hata game ya leo ni nani amemzidi Saka kucheza mpira?

Imefikia hatua mpira ukiwa kwa Saka tunafeel comfortable kuliko hata ukiwa kwa senior players.
itabidi nirudishe utamaduni wangu wa kuangalia mechi zote za big 6, huyu saka ni mara yangu ya kwanza kumuangalia.

mchezaji aliyenivutia leo ni gabriel Magalhães, naye ni mara yangu ya kwanza kumuangalia ila nimeona chembe chembe za mwendawazimu chiellini
 
Baadhi ya mashabiki mnaolaumu na kuponda performance ya timu mnakosea sana.

Arteta is a promising coach aaminiwe na kupewa anachotaka mwakani Arsenal haitashikika.

Build up ya timu ni nzuri sana tofaut na awali na shida kidogo ipo kwa kiungo na utulivu mbele, kiasi flan kulikua na presha ya wachezaji ila naamini hali itapoa. Arteta apewe mida.

Jamani mpira ni Sanaa sio kukurupuka tu eti umfunge city na liver kirahisi nao wanamjua Arteta na Arsenal yake ndo maana nao wanakaza we need Patience. Arteta apewe muda.

Tumefungwa Mechi mbili na big team zinazocompete mashindano ya kimataifa na zimefikia mbali hadi fainali misimu miwili kama si mitatu nyuma na zimewekeza heavy wewe kocha wetu kapewa timu katikati ya msimu ulioisha unataka ghafra tu bin vuu uzifunge? My friend tuwe serious

Sisi saizi zetu ni chelsea, Man U, Tot, Everton Leicester kwa msimu huu hizo zingine mbili itokee tu ila level zao bado but hawa wengine tunawamudu.

Mwisho mashabiki wengi nje na baadhi wa arsenal walijua tunakufa nyingi ila kwa matokeo Haya na mpira ulivyokua wamekua surprised na hakika wanaiogopa Arsenal moyoni mwao wanajua ila hawawezi kusema. Unabisha? Muulize shabiki wa Chelsea au Man U kama anataka kukutana na arsenal hii na awe mkweli tu.

Top four bila ajizi tumo na mwakani Uefa tunashiriki. Tushukuru kwa kila hatua tusiwe watu wa kulaumu tu.

Inaendelea.....
Tupo pamoja sana mkuu.

Na hapa ndio tunawaambia wale wote walio na unrealistic expectations basi wajiangalie. Eti tunazungumzia ubingwa.

Haya kazi kwenu Sisi wengine tuko vizuri.
 
Ukiwakuta wanakuchambulia hiyo kiungo yao yaan huyo ceballos unaweza sema labda ni boonge la mchezaj kumbe waongowaongo tu mara hapa akae xhaka pale muweke El neny yaan full vurugu tu

Nataka na huyo patei sijui part aanze kucheza tujue kama wamepigwa kama walivyopigwa kwa komred kipepe
Hatari mkuu. Mimi gunners lakini gunners wenzangu wamezidi aiseeee duh! Yaani utadhani tunachkua kombe keshoo saa mbili na robo asubuhi

😀😀😀😀😀😀
 
itabidi nirudishe utamaduni wangu wa kuangalia mechi zote za big 6, huyu saka ni mara yangu ya kwanza kumuangalia.

mchezaji aliyenivutia leo ni gabriel Magalhães, naye ni mara yangu ya kwanza kumuangalia ila nimeona chembe chembe za mwendawazimu chiellini
Yupo vizuri mkuu, Arsenal tukienda mbele huwa tuna madhara sana ila shida hatuendi mbele kwenye hizi big games,ndio ile unakuta foward line yote shot on goal hakuna yani zero kabisa, inaumiza sana.
 
Kwa anayejua Arsenal ilipotoka na ilipo sasa Hawez kubeza tulivyocheza Leo

Haya ni maneno ya Arteta

Arteta anajivunia kile Arsenal imefanikiwa.

"Lazima niseme na ninafurahi sana nimekuwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo hapa kwa miaka 4 na najua ni kiasi gani inachukua timu kufanya kile tulichofanya usiku wa leo."
 
itabidi nirudishe utamaduni wangu wa kuangalia mechi zote za big 6, huyu saka ni mara yangu ya kwanza kumuangalia.

mchezaji aliyenivutia leo ni gabriel Magalhães, naye ni mara yangu ya kwanza kumuangalia ila nimeona chembe chembe za mwendawazimu chiellini
Watch the kid, he is a wonderful lad.

Saka has been playing so well for a while now
 
Back
Top Bottom