Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tumecheza fresh tu,ila tatizo letu ni kuchukua muda mwingi kufanya 'build up',

Auba na pepe hawakua na wakati mzuri kutokana na uchache wa pass za mwisho za kuwafanya wascore,

Ule upande wa saka na Tierney wamecheza vuzuri Sana kuliko wakati wowote ule, Tierney alikua solid 'kinyama',saka alikua na pace ya kutosha,

Juu ya yote,wenzetu wana 'quality players' kutuzidi.
 
Tumecheza fresh tu,ila tatizo letu ni kuchukua muda mwingi kufanya 'build up',

Auba na pepe hawakua na wakati mzuri kutokana na uchache wa pass za mwisho za kuwafanya wascore,

Ule upande wa saka na Tierney wamecheza vuzuri Sana kuliko wakati wowote ule, Tierney alikua solid 'kinyama',saka alikua na pace ya kutosha,

Juu ya yote,wenzetu wana 'quality players' kutuzidi.
Kila siku tunajifariji kwa misemo hii second match vs big 6 away results o point
 
Manchester city 1-0 Arsenal Full Time nlisema before Match started

Hii timu imerogwa na aliyeiroga Wenger ndo anayemjua!No excuse at all! Kila mechi ya away vs big 6 tunapoteza!

Mechi za Away dhidi ya Manchester United Spurs Chelsea Leicester na Everton Naapa hatutaambulia kitu
Mimi kazi yangu kuweka screenshot tu.

Hapa naķupinga big time. Have faith
 
Mimi kazi yangu kuweka screenshot tu.

Hapa naķupinga big time. Have faith
Endelea kuweka na Mimi ntakuwa nakukumbusha nilisema kabla match haijaanza na yametimia aliyeturoga Wenger ndo anamjua hakuna kocha wa Arsenal aliyeshinda away tangia Wenger asepe kama yupo nikumbushe may be nimesahau nipo tayari unikosoe

Nachojua ni 2015 mara ya mwisho katika EPL ndio tumeshinda away vs Big 6 (shit)
 
Saka and Gabriel were both excellent. Xhaka had strong moments, as did Ceballos, showing that they could work very well with Partey in a three. That extra body would make a big difference away against the top six.
 
Baadhi ya mashabiki mnaolaumu na kuponda performance ya timu mnakosea sana.

Arteta is a promising coach aaminiwe na kupewa anachotaka mwakani Arsenal haitashikika.

Build up ya timu ni nzuri sana tofaut na awali na shida kidogo ipo kwa kiungo na utulivu mbele, kiasi flan kulikua na presha ya wachezaji ila naamini hali itapoa. Arteta apewe mida.

Jamani mpira ni Sanaa sio kukurupuka tu eti umfunge city na liver kirahisi nao wanamjua Arteta na Arsenal yake ndo maana nao wanakaza we need Patience. Arteta apewe muda.

Tumefungwa Mechi mbili na big team zinazocompete mashindano ya kimataifa na zimefikia mbali hadi fainali misimu miwili kama si mitatu nyuma na zimewekeza heavy wewe kocha wetu kapewa timu katikati ya msimu ulioisha unataka ghafra tu bin vuu uzifunge? My friend tuwe serious

Sisi saizi zetu ni chelsea, Man U, Tot, Everton Leicester kwa msimu huu hizo zingine mbili itokee tu ila level zao bado but hawa wengine tunawamudu.

Mwisho mashabiki wengi nje na baadhi wa arsenal walijua tunakufa nyingi ila kwa matokeo Haya na mpira ulivyokua wamekua surprised na hakika wanaiogopa Arsenal moyoni mwao wanajua ila hawawezi kusema. Unabisha? Muulize shabiki wa Chelsea au Man U kama anataka kukutana na arsenal hii na awe mkweli tu.

Top four bila ajizi tumo na mwakani Uefa tunashiriki. Tushukuru kwa kila hatua tusiwe watu wa kulaumu tu.

Inaendelea.....
 
Hahaha, unaweza kuogopa kuingiza timu uwanjani.
Ukiwakuta wanakuchambulia hiyo kiungo yao yaan huyo ceballos unaweza sema labda ni boonge la mchezaj kumbe waongowaongo tu mara hapa akae xhaka pale muweke El neny yaan full vurugu tu

Nataka na huyo patei sijui part aanze kucheza tujue kama wamepigwa kama walivyopigwa kwa komred kipepe
 
Habari washika bunduki wenzangu.
Natumai hamjambo wote .
Niseme machache kuhusu game ya leo.
Tumepoteza hii game na mazingira ya kupoteza kwetu ni wazi bado timu yetu haijawa na defence nzuri zaidi.

Timu ina viungo wazuri hata washambuliaji pia ni wazuri.Kwa mwendeleo huu ni wazi tuna timu ya ushindani compared na ya msimu uliopita.Tumekosa beki za kupandisha timu hali inayopelekea kiungo kama Xhaka kucheza kama beki na kujaribu kupandisha timu hivyo kati panapwaya hivyo tukipata beki ya kupandisha Xhaka ataitendea haki nafasi ya ukiungo.
Tumecheza na timu bora ambayo ina maumivu ya kichapo kutoka kwetu lakini pia mara nyingi tumekuwa tunafungwa goli nyingi tukutanapo na City kitu ambacho sasa hakipo kabisa.

Arteta amefanya kazi Guardiola hivyo mbinu zake nyingi za Siri anazijua na hivyo arteta ni mweupe kwa Guardiola hivyo timu lazima icheze jihad na akili sana.

Mwisho Partey ni mashine ya kazi na tutafika mbali.Ipo timu msimu huu itakula 7 mbele ya Arsenal.


We are the gunners forever and we love our team.

Mungu tubariki washika bunduki tuendelee kuwa wamoja na wenye upendo daima.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
nadhani bajeti inawaangusha arsenal, kiufupi walihitaji wachezaji wengine japo wawili wenye ubora hususan kwenye safu ya ushambuliaji.
saka, nketiah na hata pepe ni wachezaji wanaopaswa kuanzia benchi.

Acha waendelee kuteseka, maana wakishinda vimechi vya yale makombe ya mbuzi hatupumui kwenye threads zetu.
 
Back
Top Bottom