Ninatafutia mkate wangu Makumbusho na ninaishi Boko Ili niangalie mechi usiku wazia narisk vingapi? So leo ni nina hasira huku akili ipo hoi.
Na muda wote nipo kwenye purukushani za magari nawaza zile miss mbili za Lacazette, sasa hivi huko alipo atakua anawaza nini? Striker kamili unakosaje kuscore katika near identical chances?
Timu yetu ilikua hoi yet among huo uhoi some individual thought "No lets go down fighting" wanakuletea mpira kisha unafanya ujinga? Nimezoea kuona strikers wawili wanaokosa wakibaki na kipa, Rashford na Tammy leo huyu kajileta kwenye group hili.
Xhaka kama ana kutu mwili mzima, Niles, Tierney wote hawajaperform katika expected performance. Nilisema Willian hung'aa mechi moja na kupotea zijazo. Leo imejidhihirisha na mechi iliyopita imejidhihirisha.
Arteta alisema hagombei kikombe chochote lakini sikutaraji performance iwe hivi hata nilivyoandika juu ya possession kona n.k. sikudhania itakua katika hali hii.
Leeds alipata goli 3 kwa Liva. Arsenal tumepata moja na nafasi mbili kaharibu striker so Leeds ana finishing nzuri kuizidi Arsenal inapokuja juu ya kucheza na Liva. Nilisema the only way Leeds secured those goals ni kwakua waliubeba ugomvi mpaka mlangoni kwa Liva nikasema tuliopt kustay tulivyokutana nao maajabu tukashinda.
Leo tumeopt kustay na tumeonyeshwa ni jinsi gani ulikua ni uamuzi wa kijinga.
Katika point 12 tumeshapoteza 3. Tuone tutasecure ngapi kati ya zilizobaki.
Lacazette mjinga sana.
On to the next one.