Nketiah anabadilika attitude na kua shit?
Move ya goli la kwanza dhidi ya Leicester ilianza kwa Nketiah kumpa pasi Pepe, Pepe akadrible mpaka ndani ya box na kupiga low cross ambayo iliblokiwa.
Palepale Nketiah akaonyesha kuudhika na kumuonyesha Pepe ishara ya 'Ungeuleta hapa' muda huo move bado inaendelea Pepe anapambania ule mpira uliokua blocked. Akaupata akaupeleka tena katikati ambapo ukamgonga Fuchs na kua goli.
Kwa kasi ya ule mpira Nketiah angeugusa lingekua goli pia. So ile ilikua ni pasi.
Lakini hata baada ya kua goli bado Nketiah akaonyesha ishara ya 'Ungeuleta hapa' mimi naona huyu ameanza kua mbinafsi anaamini yeye ni muhimu kuliko timu.
Wiki nyuma ametoka kugombana na Ceballos. Hata bado hilo halijapoa jana ameleta hilo jipya. Guendouz attitude yake ndiyo inamuweka benchi, tuna Folarin Balogun, tuna Gabriel Martinell huu wakati wa kukaza na kuexcel katika nyanja zote mpaka nidhamu yeye ashaanza kuota mapembe.
Balotelli alikua kipaji pia ila tunajua leo alipo na kwanini yupo pale.