Ndugu zangu
Aaron Arsenal gspain MalcolM XII 4 3 3 ingawa gspain amepoint kua ni tiki taka lakini hii hufanya kazi vyema ikiwa formation itakua na attacking fullbacks wa uhakika, kariba ya Hakimi, Davies, Arnold, Bellerin, Marcelo n.k.
Lakini ikitokea attacking fullbacks wakabanwa ndiyo utaona Liver anapigwa, Man City atapigwa na Wolves games mbili n.k. pia hii formation hua ngumu kushinda ikitokea timu pinzani ikacheza 3 5 2. Yaani hii formation ukikutana na mid ya upinzani yenye nguvu na pumzi basi mipango ndiyo inakua imeishia hapo.
Game ya PSG na Bayern tuliona jinsi Bayern alivyokaziwa akashinda moja bila tena aliyescore ni Coman mid ilishikiliwa na Davies akabanwa haswa.
Man U alivyocheza na Barcelona msimu uliopita UCL alicheza 4 3 3 mid yake ilishikiliwa kooni mpaka Man U nzima ikarudi golini.
Binafsi naamini sababu pekee timu zenye 4 3 3 zinafungwa ni ikitokea timu pinzani zinaweka 3 5 2 mfumo ambao timu ndogo nyingi ndiyo zinautumia na ndiyo zinazisurprise timu kubwa.
Kwa Arsenal yenye strikers zaidi ya 2 naamini 4 2 2 2 au 4 3 1 2 ni best kwetu, pia formation hii ni rahisi kushambulia na kurudi kukaba kwa haraka pia inakupa uwanja wa kucheza tiki taka au kaunta ukiamua.