Tusiwe na matumaini juu ya UCL baada ya miaka 3 kama Arteta alivyosema. Alijiunga Man City 2016 alikaa pale kama kocha msaidizi na tunajua City maisha yake UCL yapoje. All the while City ikiwa inamwaga pesa kwa yeyote waliyemtaka so ilikua na quality players ambao Arteta anasema Arsenal tunakosa.
Ni ukweli hatuna quality players tukiwa nao baada ya miaka 2 tutarajie UCL? Hapana, unakutana na timu kama Atalanta au Lyon au Leipzig kisha unagundua quality siyo kila kitu. Timu inahitaji spirit, commitment na winning mentality.
Kwenye Ngao ya Hisani Arteta anasema "Tukiwa vyumba vya kubadilishia nguo niliona timu nzima ikiwa na ari ya ushindi, waliamini wanaweza kushinda" hiyo ndiyo mentality inayotakiwa. Arsenal tulikutana na Liva na unaona kabisa Liva walikua bully, wakatuua 3. Winning mentality shattered fighting spirit gone.
Niliwahi sema Diego Simeon ni kocha tunayemhitaji kwakua ana uwezo wa kuifanya timu ikacheza jihad, huu uwezo alikua nao Redknap wa Totenham pia, same na Pochetino na Emery.
Timu iliyo na quality players hua na overconfidence siyo winning mentality ila timu kama Atalanta, Lyon au Leipzig wao huwa na winning mentality na ndiyo tunayoihitaji saa hii.
Akipata quality players akakosa winning mentality tutaona itakavyokua.