Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mkuu hakuna cha ajabu naamini kwenye timu yoyote inawezekana. Ila kila kitu ni process na haya mambo yanaenda hatua kwa hatua. Anzeni na EPL kwanza then onyeshe i umwamba kwenye EL ndio mkachukue hiyo UCL. Haya mambo msidhani ni bahati tu watu wanajipanga. Angalia Pep anavyohangaika uko leo hii Arsenal eti ndani ya misimu 3 akabebe UCL? Acheni masikhara bhana

Mimi Arsenal naijua bhana mtapoteana hapa na wewe ndio utabeba lawama kwa nini timu inafanya vibaya kwa sababu unawajaza wenzio ujinga na wenyewe wanajaa kweli.
Hamna mashabiki wenye moyo kama wa Arsenal,hatujachukua kombe la EPL miaka 15,still bado tunaifuatilia timu yetu.

Nyinyi sasa mabandani mechi zenu tuna tizama sisi.
 
Emi ndio golikipa namba moja kwa sasa, naona Leno ajipange upya kwa kazi kubwa ya kufanya,Martinez yupo comfortable golini, hatujaona pengo la Leno kabisa.
Emi ni mzuri sana kwenye kucheza pasi kuliko Leno.. Anajiamini sana halafu si rahisi kupoteza.

Leno yuko vizuri sana kwenye saves.

Sasa itafikia muda, timu ikishapata wachezaji wa maana wa kugombania mataji makubwa kama UCL, tutakuwa tunahitaji kipa anaejiamini zaidi kucheza kuliko kufanya saves.. Kwa sababu muda mwingi mpira tutakuwa tukimiliki sisi.

Ni kama tunavyowaona wakina Ederson na Valdes, ni makipa wa kawaida lakini walipata/wamepata timu inayomiliki zaidi mpira. Basi wanaonekana bora wakati wote.
 
Mkuu hakuna cha ajabu naamini kwenye timu yoyote inawezekana. Ila kila kitu ni process na haya mambo yanaenda hatua kwa hatua. Anzeni na EPL kwanza then onyeshe i umwamba kwenye EL ndio mkachukue hiyo UCL. Haya mambo msidhani ni bahati tu watu wanajipanga. Angalia Pep anavyohangaika uko leo hii Arsenal eti ndani ya misimu 3 akabebe UCL? Acheni masikhara bhana

Mimi Arsenal naijua bhana mtapoteana hapa na wewe ndio utabeba lawama kwa nini timu inafanya vibaya kwa sababu unawajaza wenzio ujinga na wenyewe wanajaa kweli.
Acha kulalamika ,kila mtu anaona timu ni process ,

Hakuna guarantee ubebe EPL ndio ubebe UCL,

Liver wamekaa miaka 30 bila EPL ,lkn UCL wamebeba sana tu

Muda mwingine Kuwa na hoja ,

Acha kupiga ramli,

In Arteta we Trust , tutafungwa ila sio kizembe ,
 
Done deal! Rob #Holding to #Newcastle from #Arsenal on loan. The deal will be complete and official after #GabrielMagalhaes announce. #transfers #NUFC #AFC
 
Pierre Emerick Aubameyang turned down two bids to stay at Arsenal. [@FabrizioRomano]

My f**king Captain.
IMG_20200829_213952.jpg
 
Mkuu hakuna cha ajabu naamini kwenye timu yoyote inawezekana. Ila kila kitu ni process na haya mambo yanaenda hatua kwa hatua. Anzeni na EPL kwanza then onyeshe i umwamba kwenye EL ndio mkachukue hiyo UCL. Haya mambo msidhani ni bahati tu watu wanajipanga. Angalia Pep anavyohangaika uko leo hii Arsenal eti ndani ya misimu 3 akabebe UCL? Acheni masikhara bhana

Mimi Arsenal naijua bhana mtapoteana hapa na wewe ndio utabeba lawama kwa nini timu inafanya vibaya kwa sababu unawajaza wenzio ujinga na wenyewe wanajaa kweli.
Acha matusi...kwamba Arsenal's Fans tunaweza kujazwa ujinga kirahisi tu. Bahati mbaya werevu wako siuoni pia....
 
Naona dalili kwamba tukiendelea hivi, 2021-2022 tutakua UCL na wakutusumbua kule hatakuwepo. Labda Bayern kidogo kama ataendelea kuwa on fom 😀😀
Haahaaaa kmmk walai .....mmea ukivutia chooni hz ndo shida zake sasa
 
Niles can adapt in so many format in the team.. last 3 games in Wembley ,he has operated from the right mid field with 3 at the back. He did that well against Chelsea and yesterday against Liverpool ..we need him to in this team. He will become more valuable
IMG_20200829_213514.jpg
 
Arteta akiwaongelea Emi Vs Leno:

" Napenda kuwa na magoli kipa wenye viwango kama Bernd na Emi. Sitaki kuwafurahisha wote, Nataka ambae hachezi akasirike. Akasirike ili ajitume zaidi awe bora au apate namba kwa kufanya hivyo."

#coyg
arsenalbongo_-20200829-0002.jpg
 
Acha kulalamika ,kila mtu anaona timu ni process ,

Hakuna guarantee ubebe EPL ndio ubebe UCL,

Liver wamekaa miaka 30 bila EPL ,lkn UCL wamebeba sana tu

Muda mwingine Kuwa na hoja ,

Acha kupiga ramli,

In Arteta we Trust , tutafungwa ila sio kizembe ,
Hoja yangu unaikwepa halafu unafokafoka tu. Nakurahisishia kwa kukwambia kwamba kwa Arsenal yenu hamuwezi kuchukua UCL ndani ya miaka 3. Hata EL mpaka damu zitawatoka puani hamchukui msimu ujao.

Mtasema naongea kwa chuki ila kila kitu kinaonekana. Tukutane msimu ujao.
 
Acha matusi...kwamba Arsenal's Fans tunaweza kujazwa ujinga kirahisi tu. Bahati mbaya werevu wako siuoni pia....
Wewe mwerevu ungefanya research kwa ndugu zako uone walivyokua wanamtupia lawama mwenzenu humuhumu kwa nini timu inafanya vibaya.
 
Hoja yangu unaikwepa halafu unafokafoka tu. Nakurahisishia kwa kukwambia kwamba kwa Arsenal yenu hamuwezi kuchukua UCL ndani ya miaka 3. Hata EL mpaka damu zitawatoka puani hamchukui msimu ujao.

Mtasema naongea kwa chuki ila kila kitu kinaonekana. Tukutane msimu ujao.
Hata community shield jana mlisema hatubebi lakini tumebeba ndoo!.. Mtakasirika sana msimu huu!.. Nakuombea maisha marefu ili uone tunavyofanikiwa
 
Machache kuhusu Community Shield

1-|. Michael Arteta Katika siku 45 ameifunga Liverpool mara 2, kaifunga Manchester United mara 1, kaifunga Chelsea mara 1, na kaifunga Manchester City mara 1, amewaonea sana hawa wanaojiita top six

2-|. Ameonyesha kuwa habatishi kwenye approach yake katika hizi mechi kubwa, kuanzia kwenye upangaji wa kikosi, format ya mfumo na mbinu zake zilifanikiwa sana, kwenye mechi ya jana alijiandaa kujilinda kwanza, alimuheshimu sana mpinzani wake, na pindi alipoupata mpira timu iliondoka kwa kasi kwenda kwenye lango la mpinzani,

3-|. Aubameyang, Mechi zote kubwa huamuliwa kikubwa na wachezaji wakubwa, nafasi moja aliyoipata ilitosha kuwaadhibu Liverpool, alicheza kwa kujituma sana, tatizo pekee linalomsibu ni aina ya wachezaji anaocheza nao, hawajui wasimame wapi au wakimbie katika nafasi zipi, walimfanya Aubameyang akose machaguo mengi ya kufanya pindi anapokuwa na mpira kwenye nusu ya adui

4-|. Mohamed Elneny, unaweza kumuita Maestro, alipokea akatoa na akauomba tena mpira, ni kiungo aliyekuwa active muda wote, alikaba, aliziba njia na aliondoka na timu kwenda kushambulia, uwezo wake wa kumiliki mpira na kutoa pasi nyingi za usahihi ziliifanya idara ya kiungo ya Liverpool kulazimika kutumia nguvu kubwa kuwapora mipira Arsenal

5-|. David Luiz, Mechi ya jana alitulia sana, aliupanga vyema ukuta wake na hakukubali kufanya makosa, timu yenye Salah, Mane na Firmino ni ngumu sana kuweza kuizuia lakini chini ya Luiz alionyesha inawezekana kama ukiwa na beki kiongozi kama yeye, usiku wa jana unaweza kusema Arsenal haihitaji tena beki

6-|. Martinez, Ametusahaulisha kama yeye ni golikipa namba mbili, utulivu wake na uhodari wake wa kuzuia mipira usiguse zile nyavu ulimfanya Sadio Mane kuonekana kama Yikpe aliyenyoa, natamani niendelee kumuona kwenye mechi nyingi zaidi

7-|. Jurgen Kloop, Aliposhindwa kuiamua mechi kwenye kikosi cha kwanza kilichoanza alihitaji kuimaliza kwa kutumia wachezaji wa akiba, kibaya wajumbe walimpitisha lakini kamati kuu ikamkata,

8-|. Naby Keita, Ana vitu vingi vitamu na vinavyovutia katika miguu yake lakini hana pumzi, alipoingia alileta uhai na ubunifu mkubwa kwenye kiungo cha Liverpool, alipiga pasi nyingi sana zinazofika, aliiendesha timu na timu ikacheza kupitia yeye lakini dakika 10 za mwisho akawa amekata upepo, timu ikashindwa kwenda mbele, plan za Kloop alizoingia nazo zikafia kwenye miguu yake

9-|. Takumi Minamino, sina shida na goli alilofunga, shida yangu ni kutaka kuendelea kumuona akiaminiwa na kuanza kwenye kikosi cha kwanza, mjanja mjanja hivi halafu kama mguu wake una sumaku, alipoingia alikuja na maswali mengi kwa Hector Bellerin na Bellerin alipokosa majibu Arteta aliamua kumpumzisha

10-|. Sub ya Firmino, mpaka sasa sijui kwanini alitolewa, sikuona kama Firmino alichoka wala sikumuona Firmino akiwa nje ya mchezo, wakati ambao Keita ameishiwa pumzi ndiyo wakati ambao Firmino alitolewa, ubunifu ukafa, akakosekana mchezaji aliyepandisha timu, akakosekana mchezaji ambaye angeamua timu ipitie wapi, wakati ambao Arsenal wakihitaji kupewa presha kubwa ndio wakati ambao walitulia na kuwapa presha Liverpool

----------------------------------

David Luiz alisema aliondoka Chelsea na kujiunga na Arsenal ili ashinde makombe, wengi walimpuuza lakini sasa hivi kashabeba mawili, baada ya kushinda kombe la Community Shield katika usiku wa jana, alisikika akisema yamebaki makombe mawili, kombe la Uefa Champions league pamoja na kombe la ligi kuu England, navyowajuwa mtasema tumpeleke Milembe

IMG_20200829_212509.jpg
 
Hoja yangu unaikwepa halafu unafokafoka tu. Nakurahisishia kwa kukwambia kwamba kwa Arsenal yenu hamuwezi kuchukua UCL ndani ya miaka 3. Hata EL mpaka damu zitawatoka puani hamchukui msimu ujao.

Mtasema naongea kwa chuki ila kila kitu kinaonekana. Tukutane msimu ujao.
Umekosa tunguli tu

Lakini tayari ni mchawi 100%
 
Back
Top Bottom