AUBAMEYANG, COUTINHO, NA WILLIAN
TUTAUPATAJE UBORA WAO?
Jurgen Klopp ni kama anamwambia Mikel Arteta jinsi ya kumfanya Philippe Coutinho ni kwa vipi awe Bora, hii ni baada ya mazungumzo yanayotajwa ya kuhamia Arsenal
Kupitia Klopp Ndipo tuliuona ubora wa hali ya juu wa Coutinho , hii ilichagizwa na ubora wa kocha kumsaidia mchezaji kupandisha kiwango chake ,
Klopp Anasema
"Coutinho Alicheza nafasi yake anayopenda ya namba kumi na sisi mara chache, lakini aliweza kucheza namba nane vizuri na winger ya kushoto kwa uwezo mkubwa",
bosi wa Reds Klopp akiongea na Gazeti la Kicker mnamo Agosti mwaka jana
"Kwa sababu yeye" ana nguvu ya kutosha katika nafasi ndogo(small space), lakini pia ana kasi sana kwenye nafasi kubwa(large space)"
Utaona Coutinho anapokutana na ngome ya timu pinzani inayokaa sana nyuma na kufinya nafasi kuwa ndogo atatumia nguvu na akili kunyumbulika , pia kwenye nafasi kubwa pale timu pinzani inapocheza mpira wa kuacha nafasi kubwa anakuwa na kasi kubwa na kuweza kumpa nafasi ya kupiga na kutoa pasi.
Arteta amebadilisha kati ya mifumo 4-2-3-1 na 3-4-3 tangu ateuliwe kuwa kocha mkuu wa Arsenal, na mifumo yote miwili ingemfaa Coutinho kwani angeweza kucheza kama '10' kwenye 4-2-3-1 au kutokea kushoto kwenye 3-4-3
Walakini, gazeti la Times limedai bosi wa Gunners Mikel Arteta anamuhitaji nyota huyo wa zamani wa Liverpool kwa kusudi la kubadilisha mfumo wa 4-3-3 msimu ujao.
Hii inaweza kupendekeza mpango wa Arteta ni kumtumia Coutinho kama '8', uwezekano wa sanjari na Dani Ceballos na Thomas Partey au Granit xhaka .
Pamoja na kwamba Willian anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Emirates , anaweza kutumika kutokea Winger ya kushoto, na hivyo kumruhusu nahodha Pierre-Emerick Aubameyang kucheza katika nafasi yake ya mbele.(CF)
Vinginevyo, Arteta anaweza kutumia mbinu zaidi ambayo itaruhusu Coutinho na Willian kubadilishana majukumu., kwenye kushambulia.