Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kuna anafanya Arteta vinaanza kutia Mashaka, Kitendo cha kuviamini vile vichezaji vitatu vya kiingereza kua vinaweza kumpa matokeo, Nketiah.Nelson na Wilock ni vichezaji vya hovyo na Vivivu..

Sijui kipi kinafanya Arteta Asimpe nafasi Gab Martinell na anauwezo kuliko hivyo vitoto,. Zile Sub za Jana Zilikua za hovyo sana, Hakukua na sub ya kiufundi alifanya sub kama vile yupo kwenye mechi ya kirafiki..
 
Kaanza Nketiah,then Willock,Nelson,
wameingia dk 85
dk 94 goli,Arteta anafurahisha sana

Sijui kwa nini Martinelli hachezi ila hao nliowataja Arteta huwa hawaachi
Ana vipenda sana hivyo vitoto na havijui sijui uwa anaona nini kwao, Nimeamini kila kocha ana kaujinga ujinga ka kupenda wachezaji wabovu na kutokumbukuli mchezaji walau mmoja mwenye uwezo
 
Kinachonikera ni kukomaa na hivi vijamaa dah,kiukweli katika hao madogo anayeonekana ni talented na ana future nzuri ni mmoja tu Gabriel Martinelli kidogo na Saka lakini hao wengine wote wanastahili kuwa Preston Northend huko....
Katika umri wa Nelson,Nketia,Holding,Wilock n.k kama ni kuna mchezaji wa maana alishaanza kuonekana lakini hawa sio hadhi yetu,maana mbona wenzao kina Trent,Halland,Mason,Sancho,Mount,Kai,Fati wameshaonesha njia katika umri wao.....
Tunavumilia ujinga tu pale
 
Umenikumbusha maneno ya Rooney

Alisema kocha bora aliyemfundisha katika Career yake ni Van Gal, lakini Manager bora ni Sir Alex

SAF alijua ku motivate wachezaji, alijua ku deal na personality za wachezaji, alijua kuifanya nyumba yake kuwa katika uthabiti. SAF alikaa miaka 27 pale United lakini kila baada ya miaka kadhaa alikuwa anabadili Assistant coach (coaching aspect)

Nani mwenye mafanikio zaidi kati ya hao inajulikana
Kuna utofauti wa kuwa coach na manager.

Anaweza kuwa ni coach mzuri ila hafai kuwa Manager.

Manager mzuri anaonekana bila hata World Class player. Mifano ipo.
 
True....
Ila Arsene Wenger alikuwa ni Meneja na kocha kwa wakati mmoja..............mzee nimeamini tulikosea sana kumtoa kabla hatujapata mrithi wake sahihi
 
Nilichozungumzia mimi na unachopayuka wewe ni vitu viwili tofauti, mi naongelea wale vijana anaowaamini wakati uwezo wao mdogo, na kuna Dogo Martinell ana uwezo kuwazidi na hampi nafasi,. We unakuja kuropoka habari za fungu la usajili, tuliza mihemko kijana uwe unasoma na kuelewa
 
True....
Ila Arsene Wenger alikuwa ni Meneja na kocha kwa wakati mmoja..............mzee nimeamini tulikosea sana kumtoa kabla hatujapata mrithi wake sahihi
Arteta ni kocha mzuri hatuwezi kumunderstimate, wameprove hilo kina Sterling,Sane et al, shida ni hivi viazi vyetu viwango duni ht aje Pep atafeli tu
 
🤣🤣🤣 Yaani wewe huna bahati kila upande unaoshabikia kuna stress + stress zako binafsi si ndo balaa! Una ishije kwa style hii? Robidinyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…