BUKAYO SAKA KATIKA MAJUKUMU MAPYA CHINI YA ARTETA
The Gunners Jana dhidi ya Brentford walitumia mfumo wa 4-3-3 ,
Dani Ceballos akicheza kama kiungo wa chini au Deep lying playmaker kwa jina la kitaalamu ,na pembeni LCM(left medifield) na RCM(Right midfielder) au pacha No.8 kwa pande zote mbili, ambapo alianza Willock kama RCM na Saka kama LCM ,ni Mfumo ambao Arteta inaonekana atautunia wakati hana Mesut Ozil katika lineup yake.
Sio mara ya kwanza kwa Saka kucheza eneo hilo, wachezaji wa Gunners, Aliwahi kucheza eneo hilo dhidi ya Sheffield United, chini ya Kocha wa zamani Emery, na Arsenal kupoteza kwa bao 1-0 .
Lakini ni mara ya kwanza katika nafasi hiyo chini ya Arteta. Hii ni fursa nyingine kwa maendeleo zaidi ya Saka.
Saka alicheza kwa Dakika 45 katika eneo hilo , Nafasi ambayo kwa pale mancity mara nyingi hucheza David Silva , na kazi yake kubwa ni Ku operate -kati ya mistari ya kiungo cha mpinzani na ulinzi,
Na kukava nafasi ya mabeki wa pembeni na viungo wa kati .
Dakika 15 baada ya mapumziko, Arsenal iliongoza bao 1-0 .Na saka akicheza kama Left winger .
Silva amekuwa akifanya vizuri ndani ya Ligi Kuu katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, akiingia ndani na kuacha nafasi, na kufanya movement au mikimbio kwa kutoa pasi, ni tabia ambayo pia anayo Saka.
Tabia ya kuulinda mpira,hasa maeneo magumu,na kuulainisha mpira kwa haraka ,ni tabia inayoonekana kwa saka.
Nakumbuka siku moja nilimchukua rafiki yangu mshabiki wa Liverpool ,tukaenda kuangalia mech ya Arsenal vs Everton , alipomuona Saka the way anavyopokea mpira na kuuachia na kufanya mikimbio(movement) ,Pale pale aliniambia huyu ni mchezaji, awali aliniambia namsikia akitajwatajwa tu .
Kurudi kwa msimu huu uliosimama itavutia kuona kama Arteta alikuwa anafanya majaribio na ambayo atayatumia kwasasa au Msimu ujao .
Arteta anapenda kumtumia Aubameyang kutokea kushoto au Left wing,na ubavu huo eneo la beki akiwa Tierney kama chaguo la kwanza, iwapo anakuwa fiti.
Kwa hivyo, anaweza kuamini kuwa kubadilika kwa Saka na ufahamu wake wa nafasi hizo (LB & LW) utafaa vizuri sana akiwa na Kieran Tierny na Aubameyang , hasa ikizingatiwa jinsi Aubameyang anavyopenda kushambulia kwa kutokea pembeni na kuingia kwenye box.
Ni mapema sana Kumlinganisha na Silva ambaye ni moja kati ya wachezaji wa kigeni waliofanya vizuri ndani ya EPL ,
Walakini, Kwa Sifa alizonazo Saka ambazo zinaendana na Silva ,ni dhahiri siku za mbeleni anaweza kufikia uwezo kama wa Silva katika nafasi hiyo