Huyu jamaa kuna vitu anavyo, atatusaidia ila apewe muda na resources za kutosha.
Tatizo tunaloliona kwa sasa (ubovu wa mabeki na viungo) ulianza toka enzi za mzee Wenger. Hatukua na recruitment nzuri ya kupata watu sahii kwenye position hizo.
Timu yetu on paper inaweza kuonekana nzuri ila ukweli mchungu ni kuwa tuna wachezaji wengi wa kawaida. Ili kutoka hapo na kusahisha makosa ya nyuma, tunahitaji muda wa kuunda kikosi cha ushindani.
Hivyo ndugu zangu gunners tuwe wavumilivu, tusiweke matarajio makubwa kwa sasa. Tujipe walau misimu miwili, kwenye mpira hakuna shortcuts.
COYG, #HATUTOKI_HATUHAMI#
Sent using
Jamii Forums mobile app