Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

I don’t know about you, but I think Martinelli’s first goal was so difficult that not even Aubameyang could’ve finished that. The second goal was extremely class as well. Gabi has the intangibles to become a true monster of the game.
 
Imenichukua Muda Mchache Kukuelewa TIERNEY

UKO vizuri sana kwa Zile Krosi zako..Unavyozimimina,yaani huna Mpinzani Ubavuni Kwako..Nguvu kidogo Akili nyingiii..Unakaba na kushambulia kwa kasi..Umri wako Bdo Mdogo...

Natumaini Kuona Mengi kutoka Kwako hakika CELTIC wametutunuku..

#ARS
IMG-20191004-WA0002.jpeg
 
Huyo mbrazil ameaga kwao ,

Namtabilia makubwa sana, akianza kupata nafas EPL , soon media zitamuimba


Sijawahi kuwa na shaka na mbrazili, sio wale waingereza kina Nelson, Niles ubishoo mwingi
Hahahahaha vipi Tairone,Fraga na Wilker da Silva?

Gerson Jaja je?
 
Punguza chuki mkuu,hakuna asiyekosea .....kikubwa ninachokiona watu tuna haraka ya kuona jamaa anayafanya Yale aliyoyafanya LILLE katika muda mfupi sana.........tumpe muda ,tuwe na imani nae...

Wewe hapo ukihamia manzese Leo itakuchukua muda kuzoea vichochoro,utapotea sana,utaingia sana uwani kwa watu Ila ukishazoea aaaaaaaaaahhhhhhhh
Kakosa magoli matatu

Krosi fyongo moja.

Pasi fyongo zaidi ya moja.

Komedi ndani ya box 2.

Kwa haraka hizo ndiyo nazikumbuka.
 
Chuki tu na mihemko
Ndio maana nimekuomba takwimu ili tuchambue vzr ,

Maana hapo umeongopa kwa hayo uliyosema ,

Kwa dk alizocheza katoka na Rating 6.5

Bado pass accuracy ilikuwa nzuri


Huon kwamba unatudanganya live?
 
Acha hizo mkuu,mpira haupo hivyo ingekuwa kila nafasi watu wanaeka kambani nafikiri top scorer angekuwa na goli 100,na mpira wa miguu ungekuwa kama basketball
Yea nimewadanganya.

Samahanini.

Pepe aliscore zile shots na kile kichwa aliscore. Anao anao ndani ya box imesababisha penati moja.

Samahanini.
 
Shida ni kwamba mimi naongea ambacho nimekiona wewe unataka takwimu yaani kama vile inatakiwa nitafute takwimu kuthibitisha kua jamaa kuna magoli amekosa wakati nimeshuhudia.


Ni kweli tulistahili penati mbili ya Nelson na yake. Ni kweli jamaa overall kacheza vizuri.

Lakini je unatamani 75M icheze hivyo?
Sio haraka kihivyo mkuu muda mwingine muhimu kuvumiliana,wewe unafikiri hazard anavyocheza kule Madrid ndio 100m ile?pulisic pale Chelsea ni 60m ile? Maana hawa ukiwaangalia kwa makini hata martinelli au saka wapo juu zaidi yao kitakwimu kwa sasa ,lakini je kiujumla wao unaweza kuwafananisha katika ubora?

Tuwe wavumilivu japo kidogo ndugu zangu ....
 
Hapa kibanda umiza,mashabiki wenzetu wa Arsenal,wamehamishia kelele zao kwa Pepe.Nikawauliza Guendouzi vipi?Siwasikii mkipiga kelele siku hizi,Imekuaje?Wakabaki wanajichekesha!!!!!!Tunatafuta mtu wa kumpa lawama,kila mechi.Tuwe wavumilivu kidogo
Sahihi kabisa, watu walimsakama sana Matteo sasa hivi wameuchuna kama sio wao
 
Punguza chuki mkuu,hakuna asiyekosea .....kikubwa ninachokiona watu tuna haraka ya kuona jamaa anayafanya Yale aliyoyafanya LILLE katika muda mfupi sana.........tumpe muda ,tuwe na imani nae...

Wewe hapo ukihamia manzese Leo itakuchukua muda kuzoea vichochoro,utapotea sana,utaingia sana uwani kwa watu Ila ukishazoea aaaaaaaaaahhhhhhhh
Jamani mashabiki wa Arsenal baadhi yenu mbona mnakua hivi?

Nikisema Guendouz hana control na stamina naambiwa namchukia. Nimesema kilichotokea jana kwa Pepe naambiwa namchukia.

Shida ni nini kwani? Tusizibwe macho na hizi nne. Goli la pili la Martinell na la tatu la Willock kama hawa SL wangekua na beki kali wangeweza kuyazuia. Tungeweza kushinda zaidi, hilo lipo wazi. Nimemtaja ambaye angeweza kuongeza magoli kwa nyakati tofauti naambiwa namchukia.

Si mchezo.
 
Hahaha halafu hata kwenye tukio sikumuona labda sikua makini. Nikawa nashangaa jamaa yuko wapi maana akifikia yeye hua ni kusukuma tu na kupaniki. Tierney na Bellerin wanaonekana na wenyewe wanapenda ugomvi kama yeye kwahiyo tutegemee show za kuteteana nyingi wakiwa pamoja uwanjani.
Alienda aiseehhh yan dogo gue anapenda sana ugomvi....hapo ktk picha hajaonekana tu
 
Sio haraka kihivyo mkuu muda mwingine muhimu kuvumiliana,wewe unafikiri hazard anavyocheza kule Madrid ndio 100m ile?pulisic pale Chelsea ni 60m ile? Maana hawa ukiwaangalia kwa makini hata martinelli au saka wapo juu zaidi yao kitakwimu kwa sasa ,lakini je kiujumla wao unaweza kuwafananisha katika ubora?

Tuwe wavumilivu japo kidogo ndugu zangu ....
Sasa nimchukie Pepe ili iweje? Anachezea timu ninayoishabikia nimchukie ili iweje. Chuki ni neno gumu kweli kweli, Mustafi wakati anasababisha magoli sikuwahi kumchukia ila nilikua nasema simkubali.

Pepe bado sijasema kama simkubali ila nimeongelea kilichotokea jana. Notice kwamba hata Guendouz sijataja performance yake kwa mechi ya jana, ni kwakua kwa muda aliocheza na nafasi yake na jana timu kua moto weakness zake zimekua insignificant.
 
Back
Top Bottom