Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Hamkumaliza kulipa deni la pepe. Bado mnadaiwa £ 50 Million.
Hapa pressure zitawaua. Sisi ambao tumeizoea EPL huwa hatusemi sana mpaka zichezwe mechi angalau 10
 
Ulitaka aweke wachezaji wapi? Kwani nyie Arsenal mna wachezaji?
Huyu Unai anachokitafuta atakipata. Huwezi kufanya sub za kipumbavu namna hii ukategemea kupata hata sare.

Hii sare ya leo, Mungu alikua upande wetu. Hakuna cha maana tulichofanya kipindi cha pili. Hivi sisi ni wa kuzidiwa na Watford kweli!!!.
 
Ulitaka aweke wachezaji wapi? Kwani nyie Arsenal mna wachezaji?
Mkuu unajitoa ufahamu au ndio ushabiki?
Arsenal tuna tatizo la beki tu hilo hata mtoto wa kindergarten analifahamu ila idara nyingine tupo vizuri.
Kitu cha kushangaza kocha hadi leo hajui formation ya kucheza na hana uwezo wa kupanga timu na kufanya sub.
Kifupi kocha hajui cha kufanya.
 
Mkuu inawezekana unai akawa kocha mzuri ila kwa sasa Arsenal hatumuitaji tactic zake zimefeli.
 
Kwa mfano leo Pepe kaharibu, angetolewa Pepe ulitaka aingie nani? Ni tofauti na timu kama Chelsea Anatoka Pulisic anaingia Willian, Pedro anaingia Odoi. Kante hayupo Kovacic anaperform at a good level, Mount anatoka Barkley anaingia. Tammy anatoka anaingia Batshuay.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…