4-2-1-3 inawezekana Arsenal :
Arsenal hii ina tofauti kubwa sana na za misimu karibia 8-5 iliyopita unajua kwa nini? Ina wachezaji tofauti wenye kumudu mifumo tofauti lakini kama ukipatikana mfumo mmoja ambao kocha atauamini basi kutakua na mafanikio.
Kwa upande wangu, mfumo sahihi kwa Arsenal ni 4231 kwa nini?
Kulia na kushoto tuna mabeki wenye uwezo mzuri wa kupandisha mashambulizi na kuzuia kwa wakati hapa nawazungumzia majeruhi Tierney na Bellerin.
Kwa ambao hamja pata nafasi ya kumuona Tierney basi niwekeeni dhamana nawahakikishia akitulia kwenye timu vizuri bila majeraha atakaa kundi moja na akina Robertson wa Liverpool.
Bellerin sina haja ya kumuongelea uwezo wake una julikana.
Katikati wakitumika Xhaka na Torreira kama chaguo la kwanza itapendeza zaidi, kwa nini?
Torreira ni mzuri mno kwenye kukaba hivyo kupitia uwezo wake Xhaka atakua na uhuru wa kupanda juu kidogo kukoleza mashambulizi na kufanya kitendo chake maarufu #XhakaBoom na pia kutawanya mipira mirefu kila kona ya uwanja.
Nafasi ya Kiungo mshambuliaji ni ya Ozil kama chaguo la kwanza, Ozil ni Ozil kwa Arsenal hatuna Kiungo kama yeye na ni swala lisilo hitaji ubishi na katika mfumo huu uwezo wake unaweza kuonekana tena kutokana na kupungua kwa majukumu ya kukaba na kujikita zaidi kwenye kumwaga sumu kwa maadui.
Mbele kuna "utatu mtakatifu" Auba akitokea pembeni bado ana hatari vile vile katikati ubora wa Lacazette unajulikana kule juu kwa Pépé mi sina la kupasemea.
Leo nimeandaa approach ya huu mfumo kesho panapo majaaliwa nitakuja na faida za huu mfumo, mtondogoo nitakuja na changamoto zake.
Nakaribisha maoni, mapendekezo, marekebisho na matusi pia kwenye comments.

