Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 754
Arsenal jana imekubali dau la paundi milioni 4 za Uingereza kumsajili beki wa timu ya Sevilla ya Spain Sebastiene Squillaci. Usiku wa jana mchezaji huyo mzoefu alikuwa amekwishawasili jijini London kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake kabla hundi ya fwedha haijatolewa, na akifaulu medical hiyo atakamilisha kusaini makaratasi ndani ya masaa 48.
Mchezaji huyo anachukua nafasi ya William Gallas ambae amejiunga na watani wa jadi Tottenham HotSpurs ambayo ina makazi yake kaskazini mashariki ya jiji la London, Arsenal wapo kaskazini magharibi.
![]()
Sebastiene Squillaci.
Inatarajiwa beki ya kati ya kwanza ya Arsenal itakuwa na Sebastiene na Thomas Vermaelen, na wasaidizi au "backup" watakuwa Johan Djorou na Laurent Koscenlny.
good move to cement the defense after Gallas and Senderos departure