Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tutatoka kwa Watford kweli leo, vijana wako vizuri balaa.
Tunatoka, tukaze buti tu, jamaa wanajifanya "Kiboko Msheli" ila tukiwa vizuri nyuma hasa na midfield poa fresh mbona, mbele sina wasiwasi..
Troy Deeney hana lolote, anafikiri mpira mabavu, unakumbuka alivyotusema?!
Troy Deeney: Arsenal lack the cojones to compete with Watford via YouTube
 
Game ngumu mkuu.
 
TEAM NEWS:

Sokratis ameumia hivyo Rob Holding anaziba nafasi yake na Aaron Ramsey nae anaanza game.

Upande wa Watford, Navarro anaingia kuziba nafasi ya beki wao wa kuaminika Janmaat ambae ana tatizo la goti.

Troy Deaney anatumia sindano ili mradi acheze dhidi ya Arsenal.

Arsenal: Cech, Bellerin, Mustafi, Holding, Monreal, Torreira, Xhaka, Ozil, Ramsey, Aubameyang, Lacazette

Watford : Foster, Navarro, Catchcart, Kabasele, Holebas, Hughes, Doucoure, Capoue, Pereyra, Gray, Deeney
 
IMG_9099.JPG
 
Game limeanza na Watford wanaanza kushambuliwa na wanapata kona ya kwanza ambayo inaokolewa na Arsenal

Arsenal 0 Watford 0
 
Lacazette analambwa kiatu na Kabasele lakini haanguki na Watford wanapona.

Kama Lacazette angedondoka Arsenal wangepewa penalty.
 
Watford wanafanya kosa Lacazeteeeee yeye na kipa Foster oooh no he puts it wide.

Ilikuwa nafasi ya pekee.

Dakika ya 17

Arsenal 0 Watford 0
 
Back
Top Bottom