Arsenal Tour in Singapore
Kikosi cha Arsenal kabla hakijaanza kucheza mechi ya kirafiki na Athletico Madrid.
Nyuma kutoka kushoto: Hector Bellerin, Bernd Leno, Rob Holding, Shrokran Mustafi, Matteo Guendouzi, Emile Smith Rowe, na PierreEmerick Aubameyang.
Mbele kutoka kushoto: Reiss Nelson, Alexandra Lacazette, Sead, Kolasinac na Aaron Ramsey.
Arsenal wanacheza na Athletico Madrid na mpaka sasa kipindi cha pili goli ni 1-1
Mechi inachezwa uwanja wa taifa wa Singapore.
Athletico walianza kufunga dakika ya 36 kipindi cha kwanza goli lililofungwa na Correa baada ya kupokea mpira wa juu kutoka kwa Vietto.
Kipa wa Arsenal Leno akiwa hoi baada ya kufungwa goli la kwanza.
Mfungaji wa Athletico Madrid Correa akipongezwa na Vietto baada ya kufunga goli la kwanza.
Dakika ya 46 mchezaji mdogo wa Arsenal Smith Rowe nae akasawazisha goli hilo kwa goli safi ambalo amefunga akiwa nje ya boksi la hatari.
Mchezaji Aubameyang akijaribu mpira wa adhabu.
Picha zingine za Arsenal wakiwa ndani ya uwanja wa taifa wa Sngapore.
Vyumba vya Arsenal.
Vyumba vya Athletico Madrid.
Hali ya Wachezaji:
Wachezaji wa Arsenal wanaonekana wana furaha ya kusafiri kuwepo nchini Singapore.
Mesut Ozil na Mohamed Elneny wakiteta jambo.
Pierre-Emerick Aubameyang na Hector Bellerin wakiteta jambo.
Pierre-Emerick Aubameyang na Eddie Nketiah wakiingia uwanjani.
Mesut Ozil akiwa ametulia baada ya kusakamwa na chama cha soka cha Ujerumani.
Hali ni furaha tu ya kusafiri.