Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,636
- 25,617
Arsenal ijayo haitamwacha Hector Bellerin kama beki wa kulia, kushoto kutakuwa na Sead Kolasinac.
Mabeki wa kati atakuwa akianza Calum Chamber na Sokratis na hawa wanaonekana kwenye mazoezi wakicheza pamoja huku
Shkodran Mustafi na "Boss" Laurent Koscielny walikuwa wakifanya makosa mengi yalokuwa yakisababisha ama Arsenal kupoteza ushindi wanapokuwa wakiongoza kwa magoli au kufungwa mapema kabisa.
Lucas Torreira sawa anachukua namba 6 kiungo mkabaji na ndiyo atakuwa Gennaro Gattuso wetu.
Granit Xhaka anaweza kupoteza nafasi yake kutokana na makosa makubwa ambayo yamesababisha Switzerland itolewe kwenye kombe la dunia Arsenal wanaweza kumsajili Andre Gomez wa Barcelona na Xhaka akawa mchezaji wa akiba.
Kwenye mechi zote za WC Xhaka alikuwa kipoteza mipira katikati na hivyo kusababisha timu pinzani kushambulia na hatimae kufunga magoli kirahisi.
Kwenye mechi na Sweden, Switzerland ilikuwa ikimiliki mpira kwa asilimia 67 na Xhaka akapoteza mpira na kusababisha goli kwa Sweden.
Huko mbele inaonekana kupo sawa na Aubameyang ataongoza mashambulizi.
Pia tusubiri mechi za kujipima nguvu tunaona first 11 halisi.

[HASHTAG]#TimeForTorreira[/HASHTAG] .