Mbona mmeanza kutamani Wenger arudi kabla hata mrithi wake hajapatikana?Arteta is cheap option hasa kwenye budget,he's amatuer na sababu kubwa ya kung'ang'aniwa ni ubahili tu nawaza tu yeye mwenyewe alikosa game time kwenye misimu miwili ya mwisho sijui ata-command vipi dressing room yake naona wanaompigia debe wanakomaa kua amepikwa na Pep ivyo anatosha kuja Arsenal.
Hapa ni bora yule babu kuliko tatizo tunaloletewa,kama siku zote nitam-support yoyote yule ambae atakua kocha wetu.
Mbona mmeanza kutamani Wenger arudi kabla hata mrithi wake hajapatikana?
Umechambua vizuri sana.Nimekuelewa kwa sehemu hongera.Mkuu Sio Kwamba Makocha Wenye CV Kubwa Hawapo Wanaotaka Kuifundisha Arsenal! Wapo Kibao Kwani Almost Kila Kocha Anahamu Ya Kumrithi Wenger ili ajijengee Heshima Kupitia Title ya Wenger.
Lakini Problem Lipo Kwenye BUDGET! Kwasasahivi Kocha ambaye tayari Ameshajijengea CV nzuri Ukimgusa tu basi atakwambia Salary Yangu Ni £16m au zaidi per year (wakati Wenger mwenyewe alikuwa akilipwa £8m per year) Na atakuekea Sharti la Kimaandishi Kuwa Katika First window tu Yake umpe £200m za usajili na Second window umpe £100m ili akamilishe £300m Katika First Season Yake.
Sasa hapo ndiyo Owners Wanapopishana Kauli na Makocha World Class Wakati Utajiri uliyonayo Club Ya Arsenal Wanauwezo Hata Wa Kumng'oa Guardiola Pale Man City.
Lakini Ukimuangalia Arteta Hata Salary ya £7m per year yupo tayari na Hata Kama Hakupewa Hata senti ya usajili Katika Season nzima basi yupo tayari na kikosi hichohicho kwanini Matajiri Wasimkubali?
Mkuu Arteta ameshafocus Mbali hapo! Anataka Just kuja kuandika CV tu Arsenal ili Atambulikane Rasmi Katika Ukocha Hata kama akitimliwa Arsenal.
Kwa wapenzi wa Arsenal. Kama tumeweza kuvumilia miaka 14 chini ya Wenger naomba tutumie nguvu, imani hiyo hiyo kuvumilia miaka 14 mara 14 ijayo chini ya Mikel "no ubavu" Arteta maana inaelekea ndiye atachukuwa mikoba according to the reports
Aje tu hata huyo ateta maana hata tukiandika sana humu na uchambuzi uliotukuka bado mshahara atalipwa Management sis tutabak kukoment tu
Vieira bado ni kocha wa New York city bado hajapata kazi au interview Ufaransa. Timu inayosemekana kumtaka yeye na wengine ni Nantes sio Nice (per Espn). Nantes wapo mbioni kumtafuta kocha mpya na wanaangalia options zote.Piers Morgan alikua pioneer wa WENGER OUT kwa muda mrefu sana ila leo hii anaona kabisa movement zake hazijaleta maana yoyote kwa kitendo cha board kumpa timu Arteta.
Nimeuliza mara nyingi nini kitafuata baada ya Wenger Out,naona board inatuvua nguo ukweni mchana kweupeeee nasikia Vieira soon anakua coach wa Nice.
Vieira bado ni kocha wa New York city bado hajapata kazi au interview Ufaransa. Timu inayosemekana kumtaka yeye na wengine ni Nantes sio Nice (per Espn). Nantes wapo mbioni kumtafuta kocha mpya na wanaangalia options zote.
Nilikuwa nasapoti (bado nasapoti) kuondoka kwa Wenger. Arsenal tulikuwa stagnate chini ya Wenger for 14yrs. Soka letu limeporomoka in last 4 or 5 yrs ilikuwa ni vizuri kumove on to new era. Ndivyo maisha ya soka, biashara yalivyo. Hata hivyo hili la kumpa Arteta nina wasiwasi nalo sababu hana proven record zaidi ya kuwa msaidizi wa Pep. Arteta anaweza kuja kuwa kocha mzuri au mbaya hakuna anayejua. Watu wanadai Arteta ni very good katika tactics, analyze game play or whatever. Kama wanataka kumpa kazi kwa sababu hizo basi wanaweza kuwapa kazi hiyo watu kibao duniani. Wapo watu wengi wana hizo sifa. Tatizo la Arsenal miaka yote ni kuwa na board mbovu kama viongozi wa nchi za Afrika. Hawa kina Kroenke(family) na Ivan Gazidis watatuporomosha Championship miaka michache ijayo. Hawajui ku-run biashara ya soka. Wapo cheap kinoma. Soka la kudunduliza sumni hadi sumni limepitwa na wakati muda sana. Tusubiri tuone watakabidhi mikoba nani. Inawezekana Arteta akawa ni mmoja wa applicants to be considered.
ila hili la france kumpiga chini LACAZETTE na kumchukua giroud NAMPA heko sana kocha si kwa utumbo ule ambao laca ametufanyia ngoja aekwe rizevu kwanza akae ktk kochi aone wanaume wanavyopambana
hahaha kijana amechefukwa. Wachezaji wa dizain hii ndio wanaomba timu ifanye vibaya ili umuhimu wake uonekane.
Jana Alhamis Arteta kafanyiwa usaili na Board ya Arsenal na leo watamfanyia pia Thiery Henry aka "Vava Voom Chogo"
Kama vipi wawekwe wote Vieira, Henry na Arteta wasaidiane na kina Bould na Lehman