Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,665
- 25,688
Arsenal
Arsenal wameshusha dau na sasa Olivier Giroud anasajiliwa na Chelsea kwa pauni milioni 15 tu.
Mchezaji, Olivier Giroud ameonekana kuwa katika mazungumzo mazito na kocha wake Arsenal Wenger wakati wa mazoezi ya mwisho kabla ya kujiunga na Chelsea kwa dau la paundi milioni 35.
View attachment 687043
Mchezaji huyo rai wa Ufaransa akionekana vema kama sehemu ya kikosi kitakacho ingia uwanjani hapo kesho siku ya Jumanne kuvaana na Swansea City mchezo wa ligi kuu ya England.
View attachment 687045
Giroud atalazimika kuondoka Emirates endapo Arsenal itakamilisha usajili utakao weka rekodi ndani ya klabu hiyo wa kumnasa mchezaji wa Borussia Dortmund straika, Pierre-Emerick Aubameyang.
View attachment 687046
Wakati wa mazoezi hayo Giroud ameonekana kuwa mwenye furaha na amani akiwa na kocha wake Wenger huku wakifanyiana maskhara ya hapa na pale.
Arsenal wanafurahia ujio wa Aubameyang kutoka Dortmund ambapo watagharimika kutoa paundi milioni 55.4 huku wakitarajia kunyakuwa paundi milioni 35 juu ya uhamisho wa Giroud kwenda Chelsea.
Arsenal wameshusha dau na sasa Olivier Giroud anasajiliwa na Chelsea kwa pauni milioni 15 tu.