Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

"BIG EXPLANATION IS NEEDED FROM WENGER FOR THE LINEUP HE USED. WHAT THE F-U-K WAS THAT? EVEN MY 5 YEAR OLD SAID THIS WAS A DISASTER LINEUP BEFORE THE GAME KICKED OFF. WENGER MUST BE IN SOME KIND OF GAME FIXING."

Mkuu Nonda,

Habari za ndani kabisa ni kwamba wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wanataka Alexis Sanchez aondolewe kwenye timu hiyo kufikia Alhamisi jioni.

Inaaminika kwamba mechi ya jumapili haikuwa ya kupoteza endapo Wenger asingempanga Alexis Sanchez na kumwacha Lacazette kwenye bench.

Wachezaji wengi waandamizi akiwemo Ozil, Ramsey, Xhaka, Boss, Bellerin na kipa Petr wamempata ultimatum Arsene Wenger amwondoe Sanchez kufikia kesho jioni.

Wachezaji hao wanaamini kwamba Arsene Wenger amekuwa akimpendelea kwa kiasi kikubwa Sanchez na hivyo yeye kuchukulia kwamba anaweza kufanya lolote au hata kuanza kudekadeka.

Hata baada ya mechi ya jumapili ndani ya chumba cha kubadili jezi kulikuwa na majibizano makali baina ya wachezaji na Sanchez alikuwa amewekwa kati huku Petr akiongoza kutoa shutuma kwamba Sanchez hana nia tena ya kuchezea Arsenal.

Hivyo Sanchez kufikia kesho jioni anaweza kuwa ni mchezaji wa Manchester City ambapo meneja Pep Guadiola amekuwa akimvuta Kamba Sanchez kabla hata ya msimu wa 16/17 kuisha.

Hivyo ingawa Man City wanataka kulipa fedha taslim yaani milioni 50 lakini Arsenal wanataka wamsajili Rahim Sterling kama sehemu ya makubaliano ya kuwasajili wachezaji hao.

Timu ilopaswa kuanza mechi ni hii:

Petr, Bellerin, Kolasinac, Rob Holding na Boss

Kati alipaswa kuwa Xhaka na Ramsey, pembeni kulia Alex Iwobi, pembeni kushoto, Walcott, kati Lacazette na Ozil.

Wachezaji wa akiba walipaswa kuwa Giroud, Chamberlain, Coquelin, Monreal, Welbeck na Ospina.

Hizi ni habari za ndani kabisa yaani ni "Exclusive".
 
Hii wiki mbaya yaani mpaka kwenye habari za usajili, yaani unauza bunduki unabaki na panga, huyu mzee wenger sijui ana nia gani na sisi, yaani hafikiri hata kuongeza watu na usajili bado siku mbili.
 
furaha na majonzi lazma ukumbane navyo kwenye mpira, asa asikimbie wakati wa majonzi mana akumbuke wakati wa furaha pia upo.
Bora nawe unisaidie kumuelewesha mtani wetu Katavi kuwa majonzi na furaha huwa haviepukiki kwa wana michezo
 
Usajili Updates:

Arsenal wanaendelea na kuondoa baadhi ya wachezaji:

Alex Chamberlain jioni hii anazungumza na Liverpool baada ya kukataa kwenda Chelsea.

Kieran Gibbs ajiunga na West Brom Albion kwa ada ya milioni 7 pauni

839482220.jpg

Alex Oxlade-Chamberlain

Alex Oxlade Chamberlain anazungumza na Liverpool baada ya kukataa kuchezea timu ya Chelsea ambao jana walikubaliana na Arsenal kumsajili mchezaji huyo.

Mchezaji huyo wa kiungo wa kimataifa wa timu ya Uingereza mwenye umri wa miaka 24, hivi sasa yupo kambini na timu hiyo kujiandaa na mechi za kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018.

Alex Chamberlain anataka kucheza nafasi yake ya asili ya kiungo wa kati yaani "central midfield" ambayo Liverpool wanataka kumsajili badala ya Chelsea ambao wanataka kumtumia kucheza nafasi ya beki wa kulia.

DIeL9kUUQAAOWRW.jpg

Kieran Gibbs akiwa amevalia jezi yake mpya ya West Brom Albion.

Nae beki wa kushoto Kieran Gibbs leo amekamilisha utaratibu wa kujiunga na timu ya West Brom Albion kwa pauni milioni 7.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Uingereza mwenye umri wa miaka 27, amesaini mkataba wa miaka minne.

Gibbs nafasi yake ilizidi kuwa finu khasa baada ya kuwasili kwa beki mwingine wa kushoto Sead Kolasinac.
 
.... Nonda,
Habari za ndani kabisa ni kwamba wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wanataka Alexis Sanchez aondolewe kwenye timu hiyo kufikia Alhamisi jioni.

Inaaminika kwamba mechi ya jumapili haikuwa ya kupoteza endapo Wenger asingempanga Alexis Sanchez na kumwacha Lacazette kwenye bench.

Wachezaji wengi waandamizi akiwemo Ozil, Ramsey, Xhaka, Boss, Bellerin na kipa Petr wamempata ultimatum Arsene Wenger amwondoe Sanchez kufikia kesho jioni.

Wachezaji hao wanaamini kwamba Arsene Wenger amekuwa akimpendelea kwa kiasi kikubwa Sanchez na hivyo yeye kuchukulia kwamba anaweza kufanya lolote au hata kuanza kudekadeka.

Hata baada ya mechi ya jumapili ndani ya chumba cha kubadili jezi kulikuwa na majibizano makali baina ya wachezaji na Sanchez alikuwa amewekwa kati huku Petr akiongoza kutoa shutuma kwamba Sanchez hana nia tena ya kuchezea Arsenal.

Hivyo Sanchez kufikia kesho jioni anaweza kuwa ni mchezaji wa Manchester City ambapo meneja Pep Guadiola amekuwa akimvuta Kamba Sanchez kabla hata ya msimu wa 16/17 kuisha.
......
Timu ilopaswa kuanza mechi ni hii:

Petr, Bellerin, Kolasinac, Rob Holding na Boss

Kati alipaswa kuwa Xhaka na Ramsey, pembeni kulia Alex Iwobi, pembeni kushoto, Walcott, kati Lacazette na Ozil.

Wachezaji wa akiba walipaswa kuwa Giroud, Chamberlain, Coquelin, Monreal, Welbeck na Ospina.

Hizi ni habari za ndani kabisa yaani ni "Exclusive".
Je nimefahamu sawa kwamba Alexis ndiye aliyepanga timu iliyofungwa 4-0?
Kama si Alexis, ilikuwaje? Au kwa nini Wenger aliingiza kikosi kile cha "kuku" kukabiliana na "majogoo" ya Malafyale?
 
Usajili Updates:

Arsenal wanaendelea na kuondoa baadhi ya wachezaji:

Alex Chamberlain jioni hii anazungumza na Liverpool baada ya kukataa kwenda Chelsea.

Alex Oxlade Chamberlain anazungumza na Liverpool baada ya kukataa kuchezea timu ya Chelsea ambao jana walikubaliana na Arsenal kumsajili mchezaji huyo.

Mchezaji huyo wa kiungo wa kimataifa wa timu ya Uingereza mwenye umri wa miaka 24, hivi sasa yupo kambini na timu hiyo kujiandaa na mechi za kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018.

Alex Chamberlain anataka kucheza nafasi yake ya asili ya kiungo wa kati yaani "central midfield" ambayo Liverpool wanataka kumsajili badala ya Chelsea ambao wanataka kumtumia kucheza nafasi ya beki wa kulia.
Nini kimemfanya Alex Chamberlain kukataa mkataba wa 180000 kwa wiki na akubali 120000 kwa wiki atakayopata Liverpool?

Link Alex Oxlade-Chamberlain: Liverpool agree £40m deal for Arsenal midfielder
 
Nini kimemfanya Alex Chamberlain kukataa mkataba wa 180000 kwa wiki na akubali 120000 kwa wiki atakayopata Liverpool?

Link Alex Oxlade-Chamberlain: Liverpool agree £40m deal for Arsenal midfielder

Hataki kutumika kama mchezaji kiraka akiwa Arsenal na yeye ni CM central Midfielder.

Pia amekataa kuchezea Chelsea ambapo Conte alitaka kumtumia kama beki wa kulia kwa vile Chelsea pia wanamtaka Drinkwater kama CM wa nyongeza.

Kama ambavyo nimeeleza hapo awali kwamba hawa vijana wanataka kucheza nafasi zao rasmi iwe kwenye timu zao kama Liverpool ambao tangia akiwa Southampton walikuwa wakimvizia mpaka Arsenal walipomchukua au timu ya taifa ya Uingereza.
 
Je nimefahamu sawa kwamba Alexis ndiye aliyepanga timu iliyofungwa 4-0?
Kama si Alexis, ilikuwaje? Au kwa nini Wenger aliingiza kikosi kile cha "kuku" kukabiliana na "majogoo" ya Malafyale?

Alexis Sanchez hakuwa "full fit" hivyo angeingia kipindi cha pili hivyo kumwachia Lacazette aanze mechi kama siku ya kwanza dhidi ya Leicester.

Hivyo akamwambia Wenger kwamba anaweza kuanza mechi ilhali hayuko full fit.

Hizi timu huwa zina utaratibu uitwao "fitness test" kabla ya mechi yoyote ile hivyo mchezaji huweza kutoa maoni yake kwamba yupo fit na akapangwa kwenye mechi.

Kama si Alexis Sanchez Arsenal isingefungwa goli hizo nne bali kungekuwepo matokeo mengine tofauti.

Pili, Wenger alikosea kuanza na Nacho Monreal kama namba nne wakati inafahamika wazi kuwa Nacho Monreal ni beki wa kushoto na hawezi kucheza kama beki wa kati.

Hivyo hivyo kwa Robert Holding ambae badala ya kucheza namba 4 ambayo ndiyo aliyokuwa akichezea hata kule Bolton Wenger akampanga kucheza namba tatu yaani upande wa kushoto, wakati yupo beki Saed Kolasinac ambae alicheza vizuri dhidi ya Leicester.

Tatu, Wenger alianza na Ramsey kama DM defensive Midfielder badala ya Mohamed Elneny ambae katika mechi ya kwanza dhidi ya Leicester alianza na alicheza vizuri.

Wenger kwa sasa amesahau kabisa principles zake anapokuwa anatafuta ushindi na timu ya Arsenal ya leo si ile niliyoiona mwaka 2000 hadi 2004.

Na bodi ya Arsenal imekuwa ikimsikilza sana Arsene kwa kuwa tu anahakikisha Klabu inaingiza mapato yake ya kila mechi na yale ya masoko.

Ndiyo maana kunatakiwa mabadiliko makubwa kwenye klabu na mabadiliko hayo yatakuja lakini baada ya Wenger kuondoka.
 
Back
Top Bottom